2015... Chadema kutoshinda uchaguzi?

2015... Chadema kutoshinda uchaguzi?

muonamambo

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2010
Posts
879
Reaction score
551
Wana bodi heri ya pasaka... pamoja ya kwamba leo ni siku ya wajinga duniani... naomba tuachane na siku hiyo tutafakari mambo ya msingi kwa mstakabali wa nchi yetu...

Taifa letu limepitia Marais wanne wote kutoka chama cha CCM kwa miaka 50 Iliyopita.. Mengi yamefanya ya kujivunia na mengi ya kusikitisha kwa Taifa Tajiri kama hili... Binafsi ukiniuliza nilinganishe Mazuri VS mabaya Nitakwambia Mabaya yamezidi unga na kwamba kadri tunavyokwenda rasilmali za nchi yetu hazimnufaishi mtanzania na tunakoelekea zitachotwa zaidi na mataifa makubwa kupitia migongo wa viongozi tuliowaweka madarakani kwa kisingizio cha uwekezaji..

Taifa hili limepitia katika mikataba ya ajabu ambayo imekuwa ikalalamikiwa kutokana na usiri na unyeti unaowekwa kwa mikataba isiyo na tija kama ya madini na umeme... kisha bila kujifunza bado mikataba mingine inaendelea kuingia tena kupitia taratibu zilezile za usiri na unyeti... huku ukiangalia maslahi kwa mtanzania ni ya kutafuta kwa tochi....

Bila shaka wengi wetu nikiwemo mimi tunatamani kuwa na uongozi mwingine ili kulinusuru Taifa hili na majanga makubwa zaidi huko mbeleni.

Wengi wetu tunaamini kwamba labda CHADEMA wanaweza kututoa kwenye makucha haya kwa mtindo wa mfumo wa chaguzi tulizonazo sasa.. Lakini tumesahau CCM imekiri hadharani kwamba hawatakuwa tayari kuachia nchi kwa CHADEMA .. Rejea hotuba ya mwekiti/ Rais kwa NEC....

Mfumo wa chaguzi tulizonazo unategemea 100% weredi wa tume za uchaguzi.. ambazo kwa katiba ya sasa uongozi wake unachaguliwa na Rais aliyeopo madarakani ambaye ameapa kutokukabidhi nchi kwa wapinzani...

Suala la katiba liko kwenye mchakato na kwa makusudi kabisa halitakuwa limekuwa tayari kabla hatujaenda kwenye uchaguzi 2015. N a hata kama tutapata katiba mpya bado suala la kupata TUME HURU YA UCHAGUZI ni questionable!!!!!

Experience kutoka kenya imeonyesha TUME walioitegemea kuwa ni HURU imeonyesha degree kubwa ya kulalia upande mmoja na vioja vyingi vya kuchafua demokrasia..
Nashauri
  1. kama chadema wanataka hata kufikiria kushinda 2015 waache kupoteza muda kwenda vijijini wapiganie tume huru ya uchaguzi... vinginevyo waache mbio za uraisi na waelekeze nguvu kwenye kupata wabunge wengi .. ili waende kubadilishe nguvu ya bunge kutoka rubber stamp kuwa bunge la kuisimamia serikali.
  2. CHADEMA wakisha declare hawatashiriki mbio za Urais watatupa Uhuru wa kuelekeza nguvu zetu kuchagua mgombea wa CCM mwenye kuthubutu na angalau kututoa katika majanga tulionayo[ kama wapo?]
  3. Hii itaisadia chadema kutopoteza resources kwenye kinyanganyiro cha uras na kujikita kwenye majimbo na kupata wabunge wengi zaidi.
  4. Kwani kumbuka kuwa "Its not who vote that count...... its who count the votes ....in TANZANIA..."​
 
Ikiwa vyama vya upinzani vitaendelea kudundana wenyewe kwa wenyewe kama ilivyo sasa, nadhani tusahau kuona upinzani ikulu ni kheri ushauri wa kufocus na wabunge (kubadili sheria bungeni) ukafuatwa.

Sijuwi ilikuwaje hata tukafuka kwenye situation ya sasa, ambapo kila chama cha upinzani kimamkimbia mwenzake.Wakati ni logic kama vingeliunganisha nguvu, basi mziki ungekuwa mwengine kabisa.

P:S
**Nikiwa mzanzibari naamini sera ya CDM ina mabadiliko ya mfumo wa muungano, kitu ambacho hakionekani kupewa nafasi ndani ya CCM.

**Maoni yanalenga zaidi CDM Bara, na sio visiwani.
 
Hapo kwenye "kumchagua mwana ccm atakayetutoa" sahau, bora tugaragazane nao hivihivi na tume ikifanya upuuzi they will meet us citizens. zama za kufikirika zimepitwa na wakati, now every action will be met with even powerful reaction...
 
MrFroasty .. Suala la kuungana kwa vyama kwa Sasa ni ndoto Kwani CCM imevinunua vyama vyote vidogo na kufanya viwe CCM B... Hapo Hakuna option ya CDM kuungana na yeyote... Kimbilio la wanyonge ni katiba Huru ambayo sioni hivi karibuni...
ndio maana nikapate na alternative B .. Heri nusu Shari kuliko Shari kamili
 
Babu V .. Nakubaliana nawe kuhusu Hakuna mtu ww kumwini ndani ya CCM ... Lakini pia uwezekano ww CDM kushinda uchaguzi ni Mdogo kwa tume yetu tulionayo...

Tutaishia Kumwaga damu na bado tume itasema CCM imeshinda .. Read
my signature
 
Hoja yako ina maslahi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na si hoja inayosaidia juhudi za ukombozi wa Tanzania kutoka kwenye makucha ya Mfumo Fisadi.

Leo sikutaka kupost kitu JF nikamilishe kitu kingine katika Computer nimeshindwa kujizuia kwenye hili. Nina tatizo katika vipengele vyako vilivyopo hapo chini. Ushauri wako unapotosha harakati za ukombozi kutoka Mfumo Fisadi.

Hapatakuwa na tatizo kabisa kumpata rais kutoka chama ambacho si CCM kwa sababu wananchi kwa idadi Kubwa hawaitaki CCM kwenye ngazi ya Rais.

Tatizo kubwa lililopo mbele ya Watanzania ni kupata chama cha Upinzani kitachoweza kupata idadi kubwa ya Wabunge kiweze kuunda Serikali makini, yaani kiweze kupata wabunge wenye uelewa mpana wa masuala ya maendeleo ya taifa letu, lakini ambao pia watakuwa na uzalendo wa kutosha kuruhusu adhabu ya kifo kwa rushwa.

Chadema na vyama vingine vya siasa vina changamoto kubwa hiyo ya ku-identify watanzania wanaoweza kujaza nafasi za bunge lakini wabunge ambao character types zao hi bora kulizo hizi za kina Chenge na wengine wa aina yake katika Chama kilichopo madarakani. Kwa kuwa umekitaja CHADEMA, nalazimika kuelekeza maelezo yangu kwa CHADEMA.

Kazi kubwa iliyopo mbele ya Chadema ni kuandaa Wabunge wa kuunda serikali makini. Na nikiingalia hata muda wa kufanya hili hautoshi kwa kuwa mienzi ni pungufu ya 24 hadi Serikali mpya itakiwe kuingia madarakani 2015.

A) Napinga point yako namba (1) hapo chini kwa sabu jibu la badiliko la uongozi Tanzania lipo kwenye kura za vijijini, kwa sabu huko ndiko kunakoamua kwa hakika kabisa nani anakuwa rais, nani anakuwa Mbunge. Chadema kiingie vijijini kwa ajili ya kujihakikishia kinapata rais na wabunge wa kutosha kuunda serikali makini.

B) Napinga point yako ya pili (2) kwa sabu CCM haina akiba ya watu waadilifu popote pale katika mfumo wake wa uongozi. Hiki ni chama kilichojengwa juu ya msingi wa Ufisadi, kwa hiyo yeyote atayeingina popote pale katika uongozi wa nchi hii kutoka chama hiki atakuja na Mfumo Fisadi kutoka chama hiko.

C) Nakubali chadema iongeze nguvu kwenye majimbo--na kwa maana hiyo mikoani--japo ni kwa sababu tofauti na za kwako. Wafanye hili kwa lengo la kutambua watu wenye uwezo tunaoutafuta huko katika majimbo, kupata kura za kutosha kule, ili Rais wa CHADEMA aweze kuunda serikali yenye mtawanyo mzuri wa uwakilishi kutoka nchi nzima, ukiwa umesheheni watu makini wataoruhusu adhabu ya kifo kwa kosa la rushwa.

Mwisho. Chadema waongeze kasi vijijini. Rais atapatikana pasipo ugumu. Shida ipo kwenye bunge; moja ya sababu ikiwa kwamba kuna wanaCCM fulani fulani ambao itakuwa ngumu kidogo kuwatoa katika bunge. Kazi kubwa ipo vijijini, na ndo huko nguvu ziongezwe.

CHADEMA na wananchi kwa ujumla wametiwa hofu na TISS na Polisi. Moja ya kazi kubwa iliyopo ni hawa CHADEMA na wanananchi kwa ujumla wao kupata jawabu la kudharau hofu ambayo imeletwa kwa vitendo vya Mabwepande, kung'olewa watu kucha, na lile bomu lililoua Mwandishi Iringa na wahalifu kuachwa. Bila kuishinda hii hofu ya TISS na Polisi uwezekano wa CHADEMA kuunda serikali 2015 ni ndoto.

Wana bodi heri ya pasaka...
Nashauri
  1. kama chadema wanataka hata kufikiria kushinda 2015 waache kupoteza muda kwenda vijijini wapiganie tume huru ya uchaguzi... vinginevyo waache mbio za uraisi na waelekeze nguvu kwenye kupata wabunge wengi .. ili waende kubadilishe nguvu ya bunge kutoka rubber stamp kuwa bunge la kuisimamia serikali.
  2. CHADEMA wakisha declare hawatashiriki mbio za Urais watatupa Uhuru wa kuelekeza nguvu zetu kuchagua mgombea wa CCM mwenye kuthubutu na angalau kututoa katika majanga tulionayo[ kama wapo?]
  3. Hii itaisadia chadema kutopoteza resources kwenye kinyanganyiro cha uras na kujikita kwenye majimbo na kupata wabunge wengi zaidi.
  4. Kwani kumbuka kuwa "Its not who vote that count...... its who count the votes ....in TANZANIA..."​
 
Hata raila alitegemea katiba mpya imwingize madarakani akasahau wenye mamlaka hayo ni wananchi....vivo hivyo wapinzani wa tanzania wachukue hilo somo
 
Wakati ukifika watanzania watajitokeza na mtanzania mmoja tu atakuwa rais wa nchi hii...wala hakuna haja ya kuumiza vichwa saivi, tufanye kazi
 
-Tunajadili platform ipi itakayotoa mgombea bora na si vinginevyo

-Ingekua jinsi mleta mada alivyosema basi chama cha PF Zambia kisingeshinda uchaguzi.Mazingira yote yalifanana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya sasa.

CHADEMA kinakwenda kuunda serikali mwaka 2015.
 
Hello Highlander... Napenda tujadili fact na tuache ushabiki pembeni ... Wish and fact are two different things.


Wish;
  1. wote tungependa kupata ukombozi dhidi ya utawala ww kifisadi
  2. wote tunapenda CDM wawe wemefanikiwa Kifika vijijini na wamepata Mtandao wa kutosha na kwamba watanzania wawe na moyo na kupiga kura pia kuzilinda if possible
  3. wote tungependa Chama kiwe na uwezo wa kuzunguka nchi nzima na kusimamisha wagombea Imara ndani ya kipindi cha miaka miwili kilichobaki
  4. wote tunatumaini tume ya uchaguzi itatenda haki na kutangaza washindi bila kupendela
Fact:
  1. Muda uliobaki na resources walizonazo CDM wanabidi kuamua for the best of our interest ... Kuingia kwenye uchaguzi ambao 100% tume itapndelea CCM. Hakuna haja ya kupoteza resources na Kuja kugombea a na tume kwa kugandamiza democracy..
  2. Wewe mwenyewe umekiri Muda ni Mdogo kwa CDM KU realize wabunge bora wa Kuja kuleta ushindani wa Kweli katika kila kona ... Uoni ni bora kuongeza nguvu upande mmoja na kufanikiwa zaidi kuliko kuwinda zote na kushindwa zote?
Kumbuka hapa hatukatishani tamaa tunapeana fact ili tusonge mbele... I stand to be corrected ....



Hoja yako ina maslahi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na si hoja inayosaidia juhudi za ukombozi wa Tanzania kutoka kwenye makucha ya Mfumo Fisadi.

Leo sikutaka kupost kitu JF nikamilishe kitu kingine katika Computer nimeshindwa kujizuia kwenye hili. Nina tatizo katika vipengele vyako vilivyopo hapo chini. Ushauri wako unapotosha harakati za ukombozi kutoka Mfumo Fisadi.

Hapatakuwa na tatizo kabisa kumpata rais kutoka chama ambacho si CCM kwa sababu wananchi kwa idadi Kubwa hawaitaki CCM kwenye ngazi ya Rais.

Tatizo kubwa lililopo mbele ya Watanzania ni kupata chama cha Upinzani kitachoweza kupata idadi kubwa ya Wabunge kiweze kuunda Serikali makini, yaani kiweze kupata wabunge wenye uelewa mpana wa masuala ya maendeleo ya taifa letu, lakini ambao pia watakuwa na uzalendo wa kutosha kuruhusu adhabu ya kifo kwa rushwa.

Chadema na vyama vingine vya siasa vina changamoto kubwa hiyo ya ku-identify watanzania wanaoweza kujaza nafasi za bunge lakini wabunge ambao character types zao hi bora kulizo hizi za kina Chenge na wengine wa aina yake katika Chama kilichopo madarakani. Kwa kuwa umekitaja CHADEMA, nalazimika kuelekeza maelezo yangu kwa CHADEMA.

Kazi kubwa iliyopo mbele ya Chadema ni kuandaa Wabunge wa kuunda serikali makini. Na nikiingalia hata muda wa kufanya hili hautoshi kwa kuwa mienzi ni pungufu ya 24 hadi Serikali mpya itakiwe kuingia madarakani 2015.

A) Napinga point yako namba (1) hapo chini kwa sabu jibu la badiliko la uongozi Tanzania lipo kwenye kura za vijijini, kwa sabu huko ndiko kunakoamua kwa hakika kabisa nani anakuwa rais, nani anakuwa Mbunge. Chadema kiingie vijijini kwa ajili ya kujihakikishia kinapata rais na wabunge wa kutosha kuunda serikali makini.

B) Napinga point yako ya pili (2) kwa sabu CCM haina akiba ya watu waadilifu popote pale katika mfumo wake wa uongozi. Hiki ni chama kilichojengwa juu ya msingi wa Ufisadi, kwa hiyo yeyote atayeingina popote pale katika uongozi wa nchi hii kutoka chama hiki atakuja na Mfumo Fisadi kutoka chama hiko.

C) Nakubali chadema iongeze nguvu kwenye majimbo--na kwa maana hiyo mikoani--japo ni kwa sababu tofauti na za kwako. Wafanye hili kwa lengo la kutambua watu wenye uwezo tunaoutafuta huko katika majimbo, kupata kura za kutosha kule, ili Rais wa CHADEMA aweze kuunda serikali yenye mtawanyo mzuri wa uwakilishi kutoka nchi nzima, ukiwa umesheheni watu makini wataoruhusu adhabu ya kifo kwa kosa la rushwa.

Mwisho. Chadema waongeze kasi vijijini. Rais atapatikana pasipo ugumu. Shida ipo kwenye bunge; moja ya sababu ikiwa kwamba kuna wanaCCM fulani fulani ambao itakuwa ngumu kidogo kuwatoa katika bunge. Kazi kubwa ipo vijijini, na ndo huko nguvu ziongezwe.

CHADEMA na wananchi kwa ujumla wametiwa hofu na TISS na Polisi. Moja ya kazi kubwa iliyopo ni hawa CHADEMA na wanananchi kwa ujumla wao kupata jawabu la kudharau hofu ambayo imeletwa kwa vitendo vya Mabwepande, kung'olewa watu kucha, na lile bomu lililoua Mwandishi Iringa na wahalifu kuachwa. Bila kuishinda hii hofu ya TISS na Polisi uwezekano wa CHADEMA kuunda serikali 2015 ni ndoto.
 
Kwa kuwa tumekipokea bas inamaanisha watanzania tumekiamini na tuko radh kukipa nch ifikapo 2015 kupitia sanduku la kura na kama wao{ccm} ni wataalamu wa kuiba kura sis wananch tutawaonyesha utaalumu wetu wa kulinda kura hata kwa gharama ya uhai wetu....!mungu ibark tz mungu ibarik CHADEMA....!
 
Kwa tathimini yangu CHADEMA 2015 itaunda serikali, Daftari la wapiga kura liboreshwe bila mizengwe, Tume huru ya uchaguzi, M4C kwenye majimbo hadi vijijini, Kuwa makini kuwatambua wasaliti na kuwaondoa mara moja. Ninakuambia CDM sasa hivi inakubalika hadi vijijini kuna maeneo ukivaa kijani utaonekana kama choo watu wanataka mabadiliko mimi ni wa kijijini ninakupa tathimini hii.
 
Hapo kwenye "kumchagua mwana ccm atakayetutoa" sahau, bora tugaragazane nao hivihivi na tume ikifanya upuuzi they will meet us citizens. zama za kufikirika zimepitwa na wakati, now every action will be met with even powerful reaction...

Mh! naona ushajiandaa kusema "tumeibiwaaaaaa....., tumeibiwaaaaa...tumeshinda lakini.... tumeibiwaaa....." kama kawaida.
 
Hapo kwenye "kumchagua mwana ccm atakayetutoa" sahau, bora tugaragazane nao hivihivi na tume ikifanya upuuzi they will meet us citizens. zama za kufikirika zimepitwa na wakati, now every action will be met with even powerful reaction...

Eti! Mikina Lowassa tena! Ntahama nchi!
 
-Tunajadili platform ipi itakayotoa mgombea bora na si vinginevyo

-Ingekua jinsi mleta mada alivyosema basi chama cha PF Zambia kisingeshinda uchaguzi.Mazingira yote yalifanana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya sasa.

CHADEMA kinakwenda kuunda serikali mwaka 2015.


Nakubaliana na wewe, CDM itaunda serikali kivuli 2015.
 
-Tunajadili platform ipi itakayotoa mgombea bora na si vinginevyo

-Ingekua jinsi mleta mada alivyosema basi chama cha PF Zambia kisingeshinda uchaguzi.Mazingira yote yalifanana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya sasa.

CHADEMA kinakwenda kuunda serikali mwaka 2015.


Ndugu Muonamambo ee, mgao wako wa Fact na Wishes umesahau Fact kibao.
Na falacy ya hoja yako inaanzia hapo. Kuna fact moja nimeibeba hapo juu.

Ujue Kuna Watanzania wameshaamua kwamba Rais hatoki CCM 2015. Rais atatoka mahala pengine 2015. Kila mmoja anaweza akawa na sababu tofauti na za mwenzie lakini dhamira hii naiona kila mahali ninapokwenda. Wengine ni mambo ya elimu mbovu, wengine ni mambo ya matibabu ya kutolea rushwa kuanzia dispensary hadi Muhimbili, Bugando, KCMC hadi META na Soko Matola Mbeya; wengine hawaitaki CCM na sababu kubwa ni matumizi yao mabaya ya dini ambayo wameyafanya hadi kusababisha hali kuwa tete sana nchini.

Wewe umeleta mada ambayo napenda sana kuijali. Ujue hata naacha mambo mengine muhimu hapa kwenye kompyuta kwa ajili yako.

Hizo fact zako zinapungukiwa dhamira ambayo ipo miongoni mwa watanzania. Fact hii inaelekeza kwamba tuishauri, au hata kuishawishi CHADEMA kuongeza bidii kutambua watu wataofaa kuwapo katika Serikali 2015 na kuwatengezea mazingira ya kushinda huko waliko. Hilo ni muhimu kwa sababu wananchi wapo tayari kwa mabadiliko, na tumaini lao ni CHADEMA.

Pasipokuwapo mtizamo huu CHADEMA wataingia katika Serikali Lame-duck kama Chiluba alivyofanya miaka ile pale Zambia. Watu walikuwa tayari kwa mabadiliko lakini Chama cha Chiluba hakikuwa tayari kusimamia mabadiliko ambayo wananchi walikuwa wanayataka. Ongeza dhamira ya wananchi ilivyokaa katika fact zako utagundua kwamba kinachoitajika kufanywa na CHADEMA ni kujiandaa kuunda Serikali Makini. Na hilo litawezekana tu kama Watapata idadi kubwa ya wabunge makini. And how do you do that now. Hii ndo fact napenda niione kutoka kwako.

Wewe unachofanya katika hoja yako ni kukatisha chama tamaa. Umesema "Kumbuka hapa hatukatishani tamaa tunapeana fact ili tusonge mbele... I stand to be corrected." Fact kubwa iliyopo ni kwamba Watanzania wameichoka CCM, na tumaini lao kubwa ni CHADEMA.

Chadema wanatakiwa kujiandaa kuunda serikali makini. Hata kama muda hautoshi kama ambavyo mimi na wewe tunakubaliana, bado hilo linabaki kuwa fact. Na jibu ni kuongeza bidii katika kujenga mazingira ya ushindi--hasa kwenye eneo la Bunge kwa sabu huku kwenye Urasi itakuwa kama kusukuma mlevi. Kazi itakuwa kwenye Ubunge.

Fact: M4C igangamale--mijini na vijijini. Na ni sahihi kabisa kugangamala na sera ya ku-override hofu ya TISS na Polisi. Hizi taasisi mbili ni mawe yamewekwa barabarani na CCM. Toa hayo mawe barabarani. Yanang'ang'ania, weka baruti!



Hello Highlander... Napenda tujadili fact na tuache ushabiki pembeni ... Wish and fact are two different things.


Wish;
  1. wote tungependa kupata ukombozi dhidi ya utawala ww kifisadi
  2. wote tunapenda CDM wawe wemefanikiwa Kifika vijijini na wamepata Mtandao wa kutosha na kwamba watanzania wawe na moyo na kupiga kura pia kuzilinda if possible
  3. wote tungependa Chama kiwe na uwezo wa kuzunguka nchi nzima na kusimamisha wagombea Imara ndani ya kipindi cha miaka miwili kilichobaki
  4. wote tunatumaini tume ya uchaguzi itatenda haki na kutangaza washindi bila kupendela
Fact:
  1. Muda uliobaki na resources walizonazo CDM wanabidi kuamua for the best of our interest ... Kuingia kwenye uchaguzi ambao 100% tume itapndelea CCM. Hakuna haja ya kupoteza resources na Kuja kugombea a na tume kwa kugandamiza democracy..
  2. Wewe mwenyewe umekiri Muda ni Mdogo kwa CDM KU realize wabunge bora wa Kuja kuleta ushindani wa Kweli katika kila kona ... Uoni ni bora kuongeza nguvu upande mmoja na kufanikiwa zaidi kuliko kuwinda zote na kushindwa zote?
Kumbuka hapa hatukatishani tamaa tunapeana fact ili tusonge mbele... I stand to be corrected ....
 
Ni mara mia tunyooshane hivi hivi kuliko kutosimamisha mgombea wa urais 2015 kupitia cdm

Chadema inategemewa na wananchi wengi , lazima mgombea asimame tukanyagane na ccm
 
Back
Top Bottom