2015 Chadema Isisimamishe Mgombea Urais

2015 Chadema Isisimamishe Mgombea Urais

Status
Not open for further replies.
Ukitazama hali ya siasa kwa sasa bila shaka utagundua kuwa chama tawala bado kina nguvu kubwa ambayo bado hakuna chama pinzani imara cha kuweza kupambana nayo
Chadema ndio angalau chenye nafuu kidogo kati ya vyote ila ushauri wangu kwa chama changu chadema ni kuwa kisahau kuhusu urais wa mwaka 2015 kwa kuwa bado CCM itashinda pasipo shaka yeyote

jeuri kubwa ya chama cha mapinduzi ni kuwa kina mtaji wake usio na mawaa wa watanzania wa vijijini amabao pasi na shaka wamejitolea utukufu wao kwa chama cha mapinduzi hivyo chadema hawana haja ya kutumia gharama na mudu mwingi kuwekeza katika nafasi ya urais isipokuwa wajipange vyema kwenye ubunge na udiwani
ni mwendawazimu pekee mwenye kuamini kuwa chadema ilishinda uchaguzi wa 2010
na itakuwa ni makosa tena kujipa moyo kuwa chadema itashinda tena uchaguzi wa urais 2015
badala yake chama kituandae vijana machachari ambao tumejipanga kwenda majimboni mwaka wa uchaguzi ili tuweze kuongeza idadi ya wabunge na kupata nguvu za kuwabana CCM kwenye mambo ya msingi bungeni badala ya kutumia rasilimali watu na fedha nyingi kumsapoti mtu mmoja kwenye urais ambaye matumaini ya ushindi ni sifuri

Nilikopigia mstari hapo ndio kila kitu.
 
upo sahihi,lakini huu si wakati wa kujipa moyo,maana hata Ghana chupuchupu upinzani uchukue nchi,nyakati hizi hakuna chama kinacho lala,kila chama kinafanya kazi,kila chama kina nafasi yake,ni miaka miwili tu imebaki lakini ni safari itakayokuwa na misukosuko mingi.
tuombe katiba ilete mgombea binafsi na iruhusu matokeo ya urahisi kuhojiwa mahakamani,hapo ndipo utakapo ona sarakasi za siasa.
 
Pole sana,

mkuu,huyo hazijamkaa sawa achana naye.hapa nakumbuka stori ya babu ya jamaa aliyekuwa anaogelea ziwani mara chizi akaja akachukua nguo zake na kuanza mbele.jamaa kuona hivyo akamtokea mbio akiwa uchi.sasa kimbembe babu si akaniuliza ungemdhania nani chizi kati yao kama ungewaona wanavyokimbizana?unahisi nilimjibuje...........???anyway,i was still a kid time hizo.so jiangalie
 
Mnajua kuwa CHADEMA ilishinda kwa kishindo 2010 only vyombo vya dola vikalazimisha CCM kuipa madaraka. Muulize yule Babu alie kuwa anasoma matokeo jinsi ambavyo dhamira ilivyokuwa inamsuta na kumfanya atetemeke kama anaugua kiharusi...Mpaka leo tume yako ya uchaguzi eti hawajui idadi kamili ya waliopiga kura!!!.Mkachakachua bila ya kutumia akili matokeo yake eti mnatuonyesha kuwa JK amepata kura less than 5m kati ya Watanzania 45Million! ... Mmelazimisha kuhamia Digital mkidhania kuwa mtawanyima Watanzania habari mlivyo na akili ndogo! kwa taarifa yako coming 2015 Hamtaweza kamwe kuchakachua matokeo kwani technologia itakayokuwepo itawafanya mbaki UCHI...jiandaeni angalau kwa kuwa na kikopo cha rays mlainishe njia maana dalili zote zinaonyesha mtaliwa kavukavu mpaka mrudishe matrilini zetu mlizozitoroshea ughaibuni...
 
Ukitazama hali ya siasa kwa sasa bila shaka utagundua kuwa chama tawala bado kina nguvu kubwa ambayo bado hakuna chama pinzani imara cha kuweza kupambana nayo
Chadema ndio angalau chenye nafuu kidogo kati ya vyote ila ushauri wangu kwa chama changu chadema ni kuwa kisahau kuhusu urais wa mwaka 2015 kwa kuwa bado CCM itashinda pasipo shaka yeyote

jeuri kubwa ya chama cha mapinduzi ni kuwa kina mtaji wake usio na mawaa wa watanzania wa vijijini amabao pasi na shaka wamejitolea utukufu wao kwa chama cha mapinduzi hivyo chadema hawana haja ya kutumia gharama na mudu mwingi kuwekeza katika nafasi ya urais isipokuwa wajipange vyema kwenye ubunge na udiwani
ni mwendawazimu pekee mwenye kuamini kuwa chadema ilishinda uchaguzi wa 2010
na itakuwa ni makosa tena kujipa moyo kuwa chadema itashinda tena uchaguzi wa urais 2015
badala yake chama kituandae vijana machachari ambao tumejipanga kwenda majimboni mwaka wa uchaguzi ili tuweze kuongeza idadi ya wabunge na kupata nguvu za kuwabana CCM kwenye mambo ya msingi bungeni badala ya kutumia rasilimali watu na fedha nyingi kumsapoti mtu mmoja kwenye urais ambaye matumaini ya ushindi ni sifuri

Wengine hata wakiandika maoni yao unajua kabisa hawa ndio wendawazimu
 
Hata muendelee kuwanga, hamtazuia ndoto....
 
Duh, kijana kama umeandika hii baada ya kunywa KIMPUMU, basi itakuwa imewekewa na ASPRIN. Bora ulale mapema kabla hujajinyea.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom