KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,150
Nimekua nikifuatilia kwa karibu mchakato wa kumpata mgombea urais wa marekani kwa tikiti ya chama cha republican katika uchaguzi katika uchaguzi wa marekani utakaofanyika takriban miezi minane kutoka sasa yani mwaka kesho 2012,mpaka naingia mtamboni muda huu mgombea pekee mweusi wa urais kupitia Republican muuza pizza maarufu ambae hakuwahi kuwa mwanasiasa kabla bwana HERMAN CAIN ndio anaongoza katika kura za maoni akiwa na asilimia 24% akifuatiwa na mwanasiasa na mfanyabiashara tajiri gavana Massachusetts 2003-2007 bwana MITT ROMNEY ambae ana asilimia 20%,Kama mambo yataendelea kuwa hivi upo uwezekano mkubwa wa mweusi Herman Cain kupambana na mweusi Barrak Obama kwenye uchaguzi wa marekani next year,tayari wamarekani weusi wameanza kugawanyika kufuatia dalili hizi za ushindi wa Cain huko Republican,wanaomtetea Cain ambae amekuja na tax plan ya 9-9-9 flat tax ambayo imekua ikiendelea kupata umaarufu na kukubalika kila kukicha wamekua wakijenga hoja kwamba Obama ambae anaonekana kutokuwa na mbinu za kuurekebisaha uchumi wa marekani sio mweusi kama wao kwa kuwa ana uzungu uzungu wakati Cain anawakilisha rangi ya mtu mweusi haswa hivyo wao wana kauli moja tu juu yake wanasema YES WE CAIN,wasikie wenyewe hapo chini kwenye hiyo video wanavyosema....HERMAN CAIN VS. BARACK OBAMA IN 2012 WOULD BE GREAT FOR BLACKS - YouTube
Je kama wakikutana weusi wawili hawa nani ataibuka mbabe???????????ni suala la kusubiri na kuona,but kwa maoni yangu marekani inahitaji na mabadiliko ili kuunusuru uchumi wao..naungana nao kwa kusema no more stimulus package for Obama administration no more money for obama care...YES WE CAIN!!!!!
Je kama wakikutana weusi wawili hawa nani ataibuka mbabe???????????ni suala la kusubiri na kuona,but kwa maoni yangu marekani inahitaji na mabadiliko ili kuunusuru uchumi wao..naungana nao kwa kusema no more stimulus package for Obama administration no more money for obama care...YES WE CAIN!!!!!