2002 niliopokelea mwaka huu nikiwa Selo ya polisi

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,512
Huu mwaka niliingia Lupango kwa mara ya kwanza,

Stori ipo hivi,

Disemba 2001 nimefunga shule A-level nikatua Dar, nikaona kukaa home kipindi cha sikukuu dingi alikua anabana saana, yaani kutoka kwenda kokote mwisho saa3 usiku uwe home si unajua wajeda tena?

Kwa hiyo nikaenda kwa Anko angu alikuwa ndo ana miaka3 kazini tena bachela anaishi Kinondoni. Tarehe 31.12.2001 usiku tukakubaliana na anko kuwa niende kanisani kuupokea mwaka nikitoka nimkute Tazara Club.

Nikaenda zangu Kanisani, saa 6 kama ibada imeisha nikatoka zangu church kuelekea Tazara Club jirani sana na Leaders Club, Enzi hizo Leaders ni kama ka-bar ka mtaani tu hakawiki.

Natembea zangu kupitia Bakwata, TX market, Makaburini hadi Makao makuu ya Ultimate Security pale inapoanzia Tunisia road karibu na Besta Diagnosis njia kuanzia Togo Tower ni Malaya wamejaa kila upande.

Nafika maeneo ilipo Besta sasa polisi hawa hapa, wakanisimamisha sikuhofu kwa kua sikua na wasiwasi wa uhalifu wowote. Jamaa wakanibambikiza kuwa kuna Muhindi kaibiwa simu ya 300.000, nikahoji mwizi anaibaje abaki hapohapo? wakanipiga pingu wakanipeleka kakituo kadoogo kapo karibu na Kwa Binti Madeko nyuma ya Besta hospitali, mfukoni nina sh.5200.

Kuzama ndani namkuta msela mmoja tu, baadaye kidogo wakaletwa kama8. hapo hakuna kusalimiana wala kusemeshana kila mtu anawaza namna ya kujinasua maana huna mawasiliano na mtu yoyote enzi hizo waliomiliki simu ni wachache sana tena Siemens na Phillips.

Hatujakaa sawa akaletwa msela analia kama kafiwa kazamishwa ndani kaanza kujigalagaza chini. nkajisemea "jamaa asijekuwa na mapepo?"

Akatusimulia kuwa alikuwa anatoka hospitali kumpeleka shemeji yake akiwa na kaka yake akaagizwa akafuate baadhi ya documenti home baada ya shemu kupewa kitanda (Enzi hizo hakuna bajaji wala boda), njiani wakati anarudi akakutana na changu mmoja yupo peke yake jamaa akawa ananigotiate akupige kimoja cha faster ndo akadakwa, hapo anawaza itakuwaje na anasubiriwa hospitali? Huwezi kuamini tulijikuta tunacheka baada ya yule changu ambaye aliletwa kumsikia analalamika polisi wamemkatia shanga zake. Wanawake walikuwa wanakusanywa kaunta maana selo ilikuwa moja tu.

Mida ya saa7.30 akaja Mkuu hata sijui ni nani maana alikuwa anatuita mmoja mmoja na kutuhoji. Mie nililambwa viboko kama 6 hivi na kutolewa nje yule jamaa ananiambia mwanafunzi unatembeaje usiku? Nikaenda zangu Tazara namkuta anko hana habari anagambeka tu na totozi hata sikumsimulia yaliyotokea, hapo nina maumivu ya viboko hata bia na nyama hazipandi.

Wale jamaa nliwalaani sana kwa kuuharibu mwaka wangu maana mwezi wa pili 2002 nkala Suspension Shuleni wakali nlikua mtoto mwema sana.

Mchana mwema.
 
Yaani polisi wakuachie tu hivi hivi usiku, wakuachie halafu nani adeki na kufagia kituo asubuhi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom