20 Most Influential Young People in Tanzania

Bulesi, hili sio suala la uvccm, ni suala la nani ni nani miongoni mwa vijana wetu - nani anasikika sana, anasikilizwa sana na anavuta sana.

Alaska, hii ni orodha ya awali, michango yenu ndio itachangia kuiboresha zaidi - inawezekana kabisa Thabeet na Mnyika nao ni kumi bora.

Kichuguu, fanya uchunguzi utagundua - mfano wa haraka haraka ni hao wa mitandao ya simu, wanatufanya tu-chizike na ku-cheka na simu.
 
Mimi napata tabu na neno influential.....
Wana influence nini?

Take mwanvita makamba for example ana influence nini? Tunakubali ni maarufu kwa daresalaam because she is the face of vodacom wanapotoa misaada but we don't even don't if she is in any decision making process (ppl working in decision making process in telecom industry says she aren't involved but she shows what have been decided)

Kwa mwanvita hata shoga yake mange kimambi has more influence than her....:...:)

hao wengine ndio kabisaaaaaa hata kuwasikia bado

for bang magazine to be influencial lazima iwe inachokiandika ndicho kinachofuatwa mtaani...... Does it affect the street fashion like that!?? Don't think so

hapa kaka Kama umeamua kuja na watu vijana unaowafagilia hivi
 
Gaijin, hoja zako ni nzito ila uzuri wake ni kuwa zina majibu ndani yake, soma tena Bang, angalia picha zake halafu linganisha na unachoona mitaani na kwenye vyombo vya habari. Kwa kuwa uko makini sana, utaniuliza swali la kuku na yai - Kipi kinamuakisi mwenzake? Vinaakisiana!

Abdulhalim, hata hilo nalo ni swali zuri na kama umeliuliza kwa nia njema basi jibu lake ni hili: Jamii lazima tuitambue na kuitumia mivuto hii.
 
Compareno.....
Bang linafuata trends ambazo zimetoka America and Europe Kisha Lina add a few touches limemaliza! Hakuna mtu anaesubiri kuona what's new in bang ndio avae isiyoshe hao wanaolipuka ki fashion bongo zaidi wanategemea vivazi kutoka nje ya nchi

Pili tujiulize watu wangapi wanasoma bang kula mwezi na wangapi wanakuwa influenced?

Tukizungumza fashion Millen Magese might be more influencial than Bang maana anachovaa yeye akiwa kazini ndicho kinachovaliwa na kuna riri na B na akina hao ndio Bang ina copy

(hapa nguo anazo vaa millen haijalishi kuwa si idea yake since we have given mwamvita that exception)
 
Gaijin, hoja zako zimepangika na rahisi kumuondoa mtu kwenye mstari, ila kumbuka hapa tunayemuongelea sio Bang - tunamuongelea CEO wake na mvuto wake kwa jamii ambao hauishii kwenye Bang tu na nasikia alikuwa mbioni kuanzisha Talk Show kama ya Oprah, hivi hujiulizi kwa nini Zantel imemtumia kwenye yale mabango yake au hujui kuwa wadau wa masoko/marketing wanajua umuhimu wa kutumia 'influential people'?
 
What influence they have ,or what power they got.
Wanaigwa kwa lipi?,wanasikilizwa lipi?,wanasaidia nini ? ,wanapendwa kwa nini?
Do they exercise influence as is defined to be?Ukiweka jina la kijana weka na what enfluence he/she excercise.

Mfano Mwanakijiji ni influential figure hapa Jamiiforums you cant argue about that, he is powerful .
 
wame influence nini? badhi naweza kusema kweli wana influence, nakumbukua kuna siku Eddo Mpaka ali-mquote mwanakijiji bungeni. Hao wengine ni kweli wame-influence kitu chochote? au ni njia ya kujikomba na kukikiss a..?
 
Je, umefanya utafiti katika kupata hayo majina? Ungeweza kutumia sample ya JF members ili kuangalia matokeo hayo kama ni sawa. Matokeo yako hayana 'objectivity'. Pia ni kweli hawa wana - influence nini na kwenye eneo gani la maisha? Pia utupe ushahidi wa matokeo ya wanacho - influence!! Au kutumwa fomu ya urais kuitembeza kwa ajili ya wadhamini ndio influence yenyewe hiyo?
 
Mwanamayu naona umeshahitimisha kuwa haina 'objectivity'. Halafu hapo hapo unauliza kama utafiti umefanyika. Kana kwamba haitoshi unashauri Likert scale itumike utadhani yenyewe ndio iko 'objective'. Ndugu yangu kuna mstari mwembamba sana kati ya objectivity na subjectivity.

Bongolander, naona na wewe umeshajijibu mwenyewe kuwa baadhi wana influence. Kutokujua influence ya watu sio kigezo cha kuhitimisha kuwa hawana influence. Ngoja tuanze kuweka wasifu wa vijana hawa mmoja baada ya mwingine tuone jinsi mvuto wao ulivyotanda na kutandawaa nchini.
 
Kabla hatujaendelea kuainisha maeneo ambayo vijana hao 10 wako 'influential' Tanzania, ngoja tuangalie tafsiri kadhaa za neno 'influential':

1. Having or exercising influence or power
2. One that is of considerable importance or influence
3. A person whose actions and opinions strongly influence the course of events
4. Making an important contribution to something

Mpaka hapo naamini sasa tuko mstari mmoja na wengi wenu mmeshaanza kuona maeneo ambayo vijana hao 10 ni muhimu sana hapa nchini.
 
Gaijin, hoja zako zimepangika na rahisi kumuondoa mtu kwenye mstari, ila kumbuka hapa tunayemuongelea sio Bang - tunamuongelea CEO wake na mvuto wake kwa jamii ambao hauishii kwenye Bang tu na nasikia alikuwa mbioni kuanzisha Talk Show kama ya Oprah, hivi hujiulizi kwa nini Zantel imemtumia kwenye yale mabango yake au hujui kuwa wadau wa masoko/marketing wanajua umuhimu wa kutumia 'influential people'?

Adds make people buy things they don't need. On another note: I am prety sure that Zantel targets corporate entities and not jua kali kwa hiyo no offence hoja ya Zantel is misplaced here.
 
Sasa tuanze kwa kuainisha eneo moja ambalo kila mmoja wa vijana hawa 10 amejitambulisha kama 'influential':

1. Emelda Mwamwanga - Ameweza kuanzisha na kuendesha kwa zaidi ya miaka 5 gazeti linalo-influence vijana walio na-influence nchini

2. Ridhwan Kikwete - Amefanikiwa kushiriki katika kuusimika na kuu-influence uongozi wa umoja wa vijana wa chama chenye influence

3. Constantine Magavilla - Ametumia kipaji chake cha kuandika na kunena ku-influence wananchi zaidi ya milioni 15 wanaotumia viselula

4. Zitto Kabwe - Amepanua wigo wa ushiriki wa vijana katika medani ya siasa na influence yake katika ubunge imetambuliwa na wananchi

5. Elsie Kanza - Amesuka na ku-influence mitandao ya kitaifa/kimataifa ya kiuchumi ya vijana iliyoshiriki mkutano wa ulimwengu wa uchumi

6. Yona Maro - Amekutanisha zaidi ya wadau 2000 wenye influence katika sekta mbalimbali kupitia mtandao unaogusa kila ofisi muhimu

7. Modesta Mahiga -Amehamasisha na kuwajenga vijana mbalimbali, hasa mashuleni, kuwa na uwezo wa kushindana katika soko la ajira

8. Mwamvita Makamba - Amekuza na ku-influence soko la za viselula ambalo linakadiriwa kuwagusa zaidi wa robo ya watanzania wote

9. Professor J - Bongo Flava - Amegusa nyoyo za vijana wengi kwa nyimbo zake zenye ujumbe mzito unao-influence vijana wamuitikie

10. Mwanakijiji - Ame-influence mawazo ya watumiaji wengi wa teknohama wakiwamo zaidi ya watu elfu 16 wanaotumia jamii forum

Si ajabu taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zikiwamo za kiserikali na kibiashara zinatumia 'influence' ya vijana wetu hawa kuwafikia wananchi wetu - sisi, je, tunawatumiaje?
 
Adds make people buy things they don't need. On another note: I am prety sure that Zantel targets corporate entities and not jua kali kwa hiyo no offence hoja ya Zantel is misplaced here.

Ndugu laiti ungejua jinsi jasho la jua kali linavyolipia haya makampuni! Laiti ungejua saikolojia ya soko ya kumpumbaza na kumpata jua kali - mwambie nawe ukijitahidi na kujinadi utakuwa kama hawa 'influentials'!
 
Nehemia Kyando MCHECHU...CEO NHC, former CEO CBA, ....Jamaa amekweaa bwana na umri ndo kwanza 37!!!!!!!!!
 
Ili kujiridhisha ilinibidi nipitie kijitabu changu cha kizungu kiitwacho concise oxford dictionary 10th edition nakukutana na maana hizi
influential
· adj. having great influence.
– DERIVATIVES influentially adv.
influence
· n.
1
the capacity to have an effect on the character or behaviour of someone or something, or the effect itself.
2 the power arising out of status, contacts, or wealth.
3 a person or thing with such a capacity or power.
4 Physics, archaic electrical or magnetic induction.
· v. have an influence on.
– PHRASES under the influence informal affected by alcoholic drink.
– DERIVATIVES influenceable adj. influencer n.
– ORIGIN ME (orig. in the sense ‘influx'): from OFr., or from med. L. influentia ‘inflow', from L. influere, from in- ‘into' + fluere ‘to flow'.

kwa hiyo ndugu companero naomba uniambie "kwanini mimi simo kwenye hiyo list yako nja ikichukuliwa kuwa nachangia mada zangu hapa jf inayosomwa na millions ya watazamazi na wapenzi wa jf DUNIANI KOTE"....au wewe mwenzetu unetumia kijitabu gani kupata maana sahihi ya mtoto wa makamba kuwa influential....ni maoni tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom