Sijui unamzungumzia ZB yupi maana hiyo sifa uliyompa haiendani kabisa na ZB aliyekuwa mshauri wa rais carter...."To day it is very easy to kill one million people but it is very difficult to control them"
Zbigniew Brzezinski
Huyu ndugu ndo kinara na mwasisi wa Us foreign policy....depopulation of third world countries
daah haya nduguSijui unamzungumzia ZB yupi maana hiyo sifa uliyompa haiendani kabisa na ZB aliyekuwa mshauri wa rais carter.
Marekani kwa kipindi cha miaka 30 hivi hapajawahi kuwa na rais ambaye alikuwa anaamin juu ya 'sanctity of life' kama rais carter na Brzezinski ambaye alikuwa anafundisha chuo cha harvard na kumfanya kuwa mshauri wake wa sera za mambo ya nje. ZB alikuwa mkimbizi toka poland ambapo alishuhudia madhila ya kibinadamu ambayo yalitokea kwao [pamoja na uropa yote] kutokana na vita ya 2 ya dunia.
Alikuwa anauchukia ukomonisti wa kirusi kupita kiasi na alifanya kila njia kuhakikisha kuwa urusi haijiongezi kidola zaidi ya ilipo.
Katika kipindi chake [ambapo utengenezaji wa silaha za maangamizo ulikuwa umefika mahala pabaya] alifanikisha makubaliano ya SALT2 ili kupunguza joto lililokuwepo. Vilevile katika kipindi hicho alifanya maridhiano kati ya china na marekani kwa kuitambua serikali ya china. kwa upande wa ma bwanyeye walimchukia kwani alisababisha taiwani itambulike kama sehemu ya china na mwisho wa siku china ikaweza kukalia kiti chake un ambacho kilikuwa kinakaliwa na taiwan.
Unaposema kuwa yeye ni 'kinara wa depopulation of third world' kwani katika kipindi chake pamoja na rais carter, hali ya dunia ilikuwa imepoa kiasi .
Kwa kukumbuka kazi nzuri aliyofanya a, mwaka 1981 alipewa nishani ya uhuru hasa kuhuisha mahusiano kati ya US na China[ alilaniwa na mabwanyeye kwa kiasi kikubwa sana na wengine waliwahi kusema kuwa alimpotosha sana rais carter.
Malipo yote kwa mungu
RIP- ZBIGNIEW BRZEZINSKI
Kiyoya,daah haya ndugu