Kulikuwa na jamaa mmoja amekaa katika baa maeneo mageni kwake, alikuwa na kinywaji chake mbele yake na alikuwa anakiangalia kwa muda mrefu, ghafla akatokea jamaa mmoja baunsa amelewa na akiwa na demu akashika glasi ya mchizi akainywa,huku anacheka
jamaa akaanza kulia, yule baunsa akamuambia,
BAUNSA: (huku anacheka) yaani wewe mjinga kweli kukuchukulia kinywaji ndio ulie??ngoja nikununulie kingine,**** kweli wewe.
JAMAA: (huku analia) siyo hivyo ila sijui nina mkosi gani leo, maana nimeamka asubuhi nikachelewa kazini nimefika bosi akanifukuza kazi, natoka nje gari yangu imeibiwa nikenda polisi wakanizungusha tu, nikapanda tax kwenda nyumbani nimeshuka katika tax nikasahau walet na simu katika tax na dereva tax si mjui,
nimeingia ndani kwangu namkuta mke wangu amelala na kijana wangu wa kazi
nikaamua kuja bar nimekaa nafikiria jinsi ya kuepukana na balaa hili la maisha na wewe umekuja umekunywa sumu yangu.