15% ya bodi ya mikopo yapingwa kila kona

Che Mkira

Senior Member
Jul 8, 2014
117
152
Nimeikwapua sehemu. Hawa madogo kama wako serious nawaunga mkono....

TSNP: TUMEUNGANA NA LHRC KUPINGA MALIPO YA 15%.

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) kupitia kurugenzi yetu ya sheria, kama wahanga watarajiwa, tumeafikiana na mawakili wetu takribani 10, kuungana na mawakili wa kituo cha haki na sheria (LHRC) kwajili ya kwenda mahakamani kupinga malipo ya 15% kwa bodi ya mikopo ambayo awali yalikuwa ni 8%.

TSNP tunatoa wito kwa chama cha walimu Tanzania (CWT), Muungano wa wafanyakazi katika sekta ya viwanda na biashara (TUICO), Umoja wa wafanyakazi wa afya wa serikali (TUGHE), Muungano wa wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) na wadau wengine wenye maslahi na suala hili, kujitokeza na kuunganisha nguvu zetu kwajili ya kupinga ongezeko hili la 15% (zaidi ya 80%) katika vyombo vya sheria.

Tunawapongeza sana LHRC kwa jambo hili muhimu. kikao cha kuleta muafaka kitaketi kesho kutwa ya juma nne ya tarehe 28, kwenye ofisi za LHRC.

Bob Wangwe
-Mkurugenzi wa sheria TSNP
 
Ngoja tuone kama vyama vingine vitasema kitu maana safari hii wawakilishi wa makundi mbalimbali siwasikii wakitetea mambo ya msingi
 
Nilikuwa nasubiri wasomi wenzetu mliospecialize kwenye tafsiri za sheria muende mkasimame nao mahakamani maana hii ilikuwa ni aibu kwa wasomi , uliona wapi mtu akakubali kulipa zaidi ya makubaliano na wakati hiyo 8% waliitaja na kuiandika wao na wala sio sisi, iweje leo wanatugeuka, hawakuwa na akili timamu walipoamua? Waitumie kwa wanaodahiliwa kuanzia mwaka huu labda, huo unyumbu hatuuwezi, ni kudhalilishana kitaaluma,
 
Kama unakumbuka huu mchezo..
Tumefika bado? Bado
Tutafika lini? Kesho
 
Only Tanzania, mambo ya kipuuuzi na serikali ya kipumbaaaaavu kama ya juha!!!!
 
Mawakili wetu hao nao wanaogopa kukatwa 15%.Ukiingia kwenye ofisi zao utadhani ya mfalme,ukiwa na kesi acha laki tano kwanza,hao ndio wanataka makato yaende polepole.
 
Back
Top Bottom