MillionHairs
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 803
- 406
Kwa hiyo kuwa wengi wanafanya upuuzi inakupa wewe uhakika kwamba it's Ok?( pathetic) Mbona wengi tu wanaweka kucha za bandia na kope za bandia yet unasema siyo sahihi? what a double standard! answer my question, kuvaa minywele bandia ndiyo alama ya urembo kwako? Njaa zitakuuweni,mnajitoa fahamu kwa sababu ya hivyo vijisenti vya kuwavalisha wanawake wenzako minywele bandia huku mkidanganyana ni urembo. i repeat,Sorry for you
Ha ha haaa eti nina njaaa...sawa nina njaa ya mafanikio lakini siyo ya tumbo. Siwazi leo nitakula nini bali nawaza leo najisikia kula nini. Ndiyo nasema tena bila ya shaka yoyote kuwa kushonea weaving,wigs na kusuka misuko kichwani ni alama ya urembo kwani kwa mwanamke urembo namba moja ni nywele.
Pia nikuambie kuwa unarusha na kupiga ngumi ukutani...kwani huwezi kuwatenganisha wanawake na urembo...hasa urembo wa nywele! Na siyo Tanzania tu au Africa bali ni dunia mzima. Ila kama utashika fimbo au pistol mkononi na kuanza kuwapiga wauzaji wa maduka ya nywele, viwanda vya nywele vilivyopo Bongo,na wanawake wa Dar wote wanaopenda urembo wa nywele basi nitaamini hichi unachokisimamia...zaidi ya hapo naona kama unafurahisha nafsi yako tu ilihali unajuwa ukweli ni upi.
Karibu tuendelee