10 kortini kwa wizi wa Sh59.9 milioni za CRDB


Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Messages
448
Points
1,000
Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2018
448 1,000
Watu 10 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka manne ikiwemo wizi wa Sh59.9 milioni mali ya Benki ya CRDB.

Washitakiwa hao ni Abdul Mahamud, Hassan Kimangale, Deogratius Mtwale, Salim Mtandika, Geofrey Michael, Wilberth Mwasongwe, Eliuphoo Swai, Arnold Natai, Rehema Alphany na Johnson Muyanda.

Akiwasomea hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Agustine Mbando, wakili wa Serikali Faraji Nguka amedai leo Mei 17, 2019 kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Aprili 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Amedai kuwa katika tarehe hiyo, washitakiwa Mahamud, Kimangale, Mtwale na Mtandika walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka la pili inadaiwa kwamba washtakiwa Mahamud, Kimangale, Mtwale, Mtandika, Michael, Ntai, Rehema na Mayunda, Aprili 25 mwaka huu eneo la Tazara Oilcom katika ATM ya CRDB waliiba Sh. 39,940,000 mali ya benki hiyo.

Katika shitaka lingine, washitakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuiba Sh20 milioni mali ya benki hiyo.

Katika la nne washitakiwa Mwasongwe na Swai, wanadaiwa kushindwa kuzuia wizi wa fedha hizo mali ya Benki ya CRDB.

Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Mmbando alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja atakaesaini bondi ya Sh3 milioni.

Wakili Nguka alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na imeahirishwa hadi Mei 31 mwaka huu na washitakiwa wote wamepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
 
mtafuta-maisha

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Messages
1,813
Points
2,000
Age
30
mtafuta-maisha

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2016
1,813 2,000
Ukweli siyo wafanyakazi wa crdb bali ni wafanyakazi wa kampuni ya G4S yenye mkataba wa kulinda na kuweka ela atm pamoja na kukusanya na kuhifadh pesa za crdb citi bank nmb nbc nakadhalika
 
kunze

kunze

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2016
Messages
320
Points
500
Age
40
kunze

kunze

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2016
320 500
Tazara Oilcom ndiyo wapi? Halafu habari bado haijitoshelezi...
Anatulisha matango pori,nimejitahidi kuitafuta tazara oilcom,hadi muda huu nimesimama hapa azam ,sijaiona. Mwandishi,andika kitu facts siyo mihemko
 
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
14,491
Points
2,000
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
14,491 2,000
Waandishi wetu wa habari ni vimeo tu.
 
mbotoro kivoi

mbotoro kivoi

Member
Joined
Sep 11, 2017
Messages
49
Points
95
mbotoro kivoi

mbotoro kivoi

Member
Joined Sep 11, 2017
49 95
Walikua n wafanyakazi w benki au coz sio rahisi kwa mtu wa nje kufanya ivo...
 
C

charles ndagulla

Senior Member
Joined
Feb 18, 2016
Messages
166
Points
250
C

charles ndagulla

Senior Member
Joined Feb 18, 2016
166 250
Kwenye hati ya mashitaka kuna majina ya washitakiwa na anwani zao hivyo mwandishi anatakiwa aangalie mwisho wa charge Sheet inataja majina,umri,kabila,dini,kazi na eneo unalokaaa.

Naamini Mwasongwe na Swai walioshitakiwa kwa kosa la kushindwa kuzuia wizi ama kushindwa kuzuia kosa lisitendeleke watakuwa watumishi wa Moja ya Taasisi za ulinzi ama Benki yenyewe.
 
jozzeva

jozzeva

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2012
Messages
1,889
Points
2,000
jozzeva

jozzeva

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2012
1,889 2,000
Nlitaka nshangae hapo akosekane Mangi.
 

Forum statistics

Threads 1,295,846
Members 498,410
Posts 31,225,217
Top