10 Fruit Juices Good for Health

shukria mzizi mkavu! Me napenda papai na tango.Asante kwa mchango wako mzuri kwa tusoyajua kuhusu afya zetu..utabarikiwa sana
@Swts na wewe ubarikiwe inshallah.

:cheer2:mkuu keep it up kuelimisha umma.thread zako zinabamba na watu wengi huku nyumbani wanazifanyia kazi.
@GOKILI Nitashukuru wakizifanyia kazi watu mimi ndio furaha yangu asante Mkuu.

Thanx dr i l'l try to make apple juice sijawahi kunywa natural one.
Mkuu@manasa jaribu kunywa hiyo Juice ya Apple utaipenda sana inshallah.
 
mzizimkavu kweli shule ni nzuri sana ila nilkuwa naomba kama unaweza nisaidia ninatatizo na kutoka vipelele shigoni nila muda mrefu kama 3 years now nimetumia dawa mbali mabli za kisasa lakini unapona may be 2 months then inarudia sijajua tatizo nini
 
mzizimkavu kweli shule ni nzuri sana ila nilkuwa naomba kama unaweza nisaidia ninatatizo na kutoka vipelele shigoni nila muda mrefu kama 3 years now nimetumia dawa mbali mabli za kisasa lakini unapona may be 2 months then inarudia sijajua tatizo nini
@Mwanaweja Pole kwa hayo matatizo ikikutokea tena hayo matatizo tumia hii dawa hii Chukua Siki Ya Apple Kidogo Changanya Na Maji Kidogo Pamoja Na Mafuta Ya Nazi Kidogo Sana, upakae Kwenye Mapele. Pakaa Kwa kila Siku Mara Moja kwa muda wa wiki moja kisha unipe Feedback.
 
Asante sana Doctor..
Huwa natumia sana Kiwi Fruits ...
napenda kula kama lilivyo..

Kwa kweli asante sana kwa kuendesha gurudumu la JF Doctor.... :) Be bless.
 
LEO nitaongelea faida za kunywa juisi katika mwili wa binadamu.
Kuna juisi za aina mbalimbali na matumizi yake yanategemea na malengo ya mtumiaji. Inawezekana watumiaji wengi wanakunywa juisi bila kujua umuhimu au kazi yake mwilini.
Safu hii itaeleza utumie juisi gani na wakati gani na nitaeleza pia jinsi ya kutengeneza na kazi zake.

JUISI YA TIKITI MAJI


Chukua tikiti maji (Watermelon), osha kisha likate vipande na chukua nyama yake ya ndani ambayo utaisaga na kupata juisi.

Faida yake
Juisi hii ina uwezo wa kusafisha figo pamoja na njia ya mkojo yaani Urethra. Inazuia unene (Obesity) kwa kuwa na kiwango kidogo cha calories.

JUISI YA KAROTI NA APPLE


Hutengenezwa kwa kusaga matunda hayo na kukamua maji yake na maelekezo yake yapo hapo chini.


JINSI YA KUTENGENEZA

Chukua kiasi cha karoti na apple kinachotosha kutengeneza juisi kwa kiasi ulichokusudia. Anza kuandaa juisi yako kwa kuosha na kumenya karoti na apple kisha katakata katika vipande vidogo vinavyoweza kusagika kirahisi kwenye blenda. Saga mchanganyiko wako ili upate juisi. Baada ya kupata mchanganyiko wa juisi yako unaweza kuongeza asali japokuwa siyo lazima kwa kuwa matunda hayo yana sukari.


Faida yake

Juisi hii ina uwezo wa kutunza ngozi yako kwani tunda la apple linaondoa uchafu kwenye ngozi na karoti nayo kwa kutumia kirutubisho cha beta-karotini chenye uwezo wa kutengeneza vitamini A huweza kulinda na kurejesha uhai katika ngozi ambapo inaifanya ionekane nyororo.

Pia juisi hii huweza kulifanya tumbo lako kuwa safi kwani husafisha tumbo na kuondoa uchafu tumboni. Aidha, juisi hii inafanya ini lifanye kazi yake vizuri kwa kulainisha nyongo na kusaidia kuondoa uchafu.

JUISI YA VIAZI MVIRINGO

Chukua viazi mviringo vinavyotosha kwa juisi. Andaa kwa kuviosha na kumenya kisha katakata vipande vidogo kwa ajili ya kuvisaga. Saga ili upate juisi uliyoikusudia.


Faida yake


Juisi hii inatumika kama dawa ya kuondoa au kupunguza asidi au gesi tumboni. Juisi ya viazi mviringo inaweza kusaidia kupunguza matatizo ya figo, kisukari, unene au kitambi.


JUISI YA MBOGAMBOGA

Juisi hii ina mchanganyiko wa mbogamboga ambazo mtumiaji hupenda kama vile matango, karoti na nyanya. Maandalizi yake ni kama juisi nyingine.

Anza kwa kuosha mbogamboga hizo kisha menya na kukatakata vipande. Saga mchanganyiko huo kwenye blenda ili upate juisi uliyoikusudia.

Faida yake

Juisi hii inasaidia kuzuia kansa hasa ile ya kwenye mfumo wa kumeng`enya chakula, kukinga mapafu na mishipa ya artery. Pia inasaidia kuimarisha kinga.
Kwa aina hizo chache za juisi unaweza kujua umuhimu wa juisi za matunda na mbogamboga tunazotumia. Kwa leo ninaishia hapo, siku zijazo nitaendelea kukupatia ufahamu kwa aina zingine za juisi pamoja na kazi zake.
 
Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki.

Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini:


KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO

Juisi ya mchanganyiko wa karoti, kitunguu swaumu na epo (apple) husafisha sumu mwilini na kuupa mwili nguvu.

EPO+TANGO+FIGILI
Juisi ya mchanganyiko wa tunda la epo, tango na mboga ya majani aina ya Figili (celery) hutoa kinga ya saratani, hupunguza mafuta ya kolestro mwilini na huondoa hali ya kuchafuka kwa tumbo na kuumwa kichwa.

NYANYA+KAROTI+EPO
Juisi ya mchanganyiko wa nyanya, karoti na epo huboresha rangi ya ngozi na huondoa harufu mbaya mdomoni.

CHUNGWA+TANGAWIZI+TANGO
Juisi ya mchanayiko wa machungwa, tangawizi na matango huboresha ngozi na hushusha joto la mwili.

NANASI+EPO+TIKITI MAJI
Juisi ya mchangayiko wa nanasi, epo na tikitimaji huondoa mlundikano wa chumvi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hii ina maana kwamba juisii hii ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya kibofu cha mkojo na figo.

KAROTI+EPO+PEASI+EMBE
Juisi ya mchangayiko wa karoti, epo, peasi na embe hushusha joto la mwili, huondoa sumu mwilini, hushusha shinikizo la damu na hupambana na matatizo ya kupumua.

PAPAI+NANASI+MAZIWA
Mchanganyiko wa papai, nanasi na maziwa, ambao una kiwango kikubwa cha vitamin C, E na Chuma (Iron), huboresha rangi ya ngozi na kuifanya iwe nyororo na husaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni (metabolism).

NDIZI+NANASI+MAZIWA
Nao mchangayiko wa ndizi, nanasi na maziwa una vitamin nyingi na virutubisho vingi na huondoa tatizo la ukosefu wa choo.

Kwa ujumla, juisi ya mchanganyiko wa matunda hayo ukitumiwa kama ipasavyo hutoa kinga tosha dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mwili na huweza pia kuwa tiba ya magonjwa yaliyotajwa hapo awali. Ili uone faida

za matunda katika suala zima la afya ya mwanadamu, jenga mazoe ya kula matunda hayo kabla hujapatwa na maradhi, kwani kwa kufanya hivyo utaupa mwili wako ile kinga yake ya asili ya kupambana na adui maradhi
 
Back
Top Bottom