Shughuli za upigaji kura zimechelewa kuanza katika maeneo mengi nchini Uganda. Awali ilitarajiwa kuwa vituo vingefunguliwa saa moja asubuhi, lakini kufikia saa mbili na nusu asubuhi, wapiga kura walikuwa bado hawajaanza kupiga kura. Zaidi ya raia milioni 21 wanatazamiwa kushiriki uchaguzi wa leo...