Mamlaka za afya nchini DRC zimeripoti visa 9,144 vilivyothibitishwa vya Ebola pamoja na vifo 4,410 tangu kuanza kwa mlipuko huo mwezi Mei. Kituo cha udhibiti wa magonjwa Africa CDC kimeuelezea mlipuko huo kuwa wa kasi zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya ugonjwa huo barani Afrika...