Harakati za kumsaka mahali alipo kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mbeya, Mdude Nyagali zimeendelea kushika kasi. Makada na viongozi wa Chadema wameendelea kuweka kambi kwenye ofisi za chama hicho, sasa wametangaza dau la Sh10 milioni kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa...