Katika jamii ya Kitanzania, baadhi ya mifugo kama vile mbuzi na ng’ombe hufariki wanapokula maganda ya mihogo mibichi. Hali hii huwastaajabisha wafugaji wengi, kwa kuwa mihogo hiyo huwa salama na hata tamu kwa matumizi ya binadamu, lakini inapoliwa na baadhi ya mifugo husababisha madhara...