Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM, Dk. John Magufuli, amewashangaa watu wanaokejeli safari za nje za Rais Jakaya Kikwete, akisema manufaa ya ziara hizo ni makubwa kuliko wanavyofikiri.
Amesema kupitia safari hizo, Rais Kikwete amefanikiwa kuwashawishi wafadhili kutoa misaada...