TBC 1 warusha harusi LIVE. Waziri Nape acharuka, awataka watoe maelezo ya kina

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,263
Naangalia television ya Taifa muda huu nashaangaa kukuta harusi inarushwa LIVE!

Ina maana television ya taifa haina kitu chochote cha kutuonyesha watanzania zaidi ya hiki kinachoendelea?

Inasikitisha sana kwa kweli..

=============

Wadau, kwanza naomba ku declare interest, kuwa sikubahatika kuiona hiyo live ya harusi binafsi ya mtu!. Pili mimi ni mdau wa broadcast journalism, na niliwahi kufanya kazi TBC enzi zile ikiitwa TVT, ila hapa sichangii kama an authority by as an experienced broadcast journalist!


  1. Naomba nitofautiane na wengi, kuwa TBC inaweza kuonyesha live ya kipindi chochote ambacho kinaonyeshwaga kikiwa recorded, hii ina maana kama TBC wanarusha kipindi cha Chereko, kikionyesha sherehe binafsi za watu, then mtu akifika bei, Chereko inaweza kwenda live kwenye event yoyote, iwe ni harusi, send off, kitchen party, ubarikio, au hata birthday ya mtu, provided ili live itatumia muda ule ule wa recored program, na kama itabidi ku extend time, isile muda wa more serious na relevant programs simply because mtu ana fedha za kulipia!
  2. TBC nayo japo ni kituo cha TV kama vilivyo vituo vingine vyote vya TV, nayo inayo haki ya kufanya biashara, kama TV nyingine zote zinazovyofanya biashaa, na ina kipindi cha Chereko kinachoonyesha harusi za watu, then kama mtu ana pesa kulipia, then why TBC ikatae pesa?!, lakini suala la kurusha matangazo ya live, it is not about money on who can pay, but the contents and national interests, nadhani TBC wangeirusha hiyo live muda ule ule wa Chereko na baada ya hapo vipindi vingine vikaendelea kama kawaida, sidhani kama kungekuwa na any basis ya malalamiko, kwa sababu live social events za public figures, prominent people na super stars zinafanyika kwenye tv duniani kote japo not on public TV.
  3. Dr. Buberwa nimefanya naye programs, hana tofauti sana na Renatus Mkinga, au Mchungaji Mtikila (RIP), kuhusiana na soundness of the state of their minds!, hivyo kitendo tuu cha mtu kulipia live ya harusi yake alone, kilitosha ku sound alarm kuhusu tuning a pivate function into a state function, mimi ndio ningekuwa producer, ningekuwa very careful to make sure live inahusisha kuonyesha events tuu na kamwe nisingithubutu kurusha live kitu chochote atakachoongea Buberwa..
  4. Mwisho, hili la TV ya taifa kufanya biashara linahitaji mjadala wa kujitegemea, BBC World Service, haifanyi biashaa, na haipokei tangozo lolote la mtu yoyote zaidi ya public announcements, lakini iko funded 100% na public, mtu yoyote ukiisha kanyaga tuu ardhi ya UK, unailipia BBC utake usitake!, na sisi tufike mahali, TBC yetu iwe funded 100% ili isihitaji sentano ya mtu, na kugawa majukumu into diferent channels say TBC 1 iwe ni nationa interest, TBC 2 comercial, ifanya biashara, TBC 3, elimu, TBC 4, Afya, TBC 5 kilimo, uvuvi na ufugaji, TBC 6 watoto, TBC 7 michezo, TBC 8 miziki etc, etc.

Pasco

Baada ya habari hii kuandikwa JamiiForums, Magazeti ya leo yameandika hivi;


tbc..jpg

Watu waliokuwa kwenye sherehe ya harusi iliyorushwa moja kwa moja na TBC.


Serikali imeliagiza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutoa maelezo ya kina baada ya kurusha matangazo ya moja kwa moja sherehe za harusi kwa zaidi ya saa mbili, jambo lilihojiwa na wananchi maeneo mbalimbali hasa katika mitandao ya jamii.

Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kupata malalamiko mengi kwa kile kilichokuwa kinarushwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1 cha shirika hilo linaloendeshwa kwa ruzuku kutoka Serikalini.

Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alibainisha kuwa amepokea simu za watu wengi waliokuwa wanahoji juu ya kipindi hicho, hivyo kulazimika kuchukua hatua mara moja za kutaka maelezo kutoka kwa watendaji wa shirika hilo.

Miongoni mwa programu za burudani na masuala ya kijamii, kituo cha TBC1 kinacho kipindi cha Chereko ambacho hurushwa kila Jumapili kwa matukio ambayo yamerekodiwa, lakini hali ilikuwa tofauti juzi usiku baada ya sherehe za harusi hiyo kurushwa moja kwa moja.

Kwa urefu wa muda uliotumika kurusha sherehe hizo, watazamaji wengi walishikwa na butwaa hivyo kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii wakihoji inawezekanaje kwa TBC1 kutoa muda mrefu kwa mtu mmoja kwa ajili ya shughuli yake binafsi.

Mtu hawezi kuitumia Televisheni ya Taifa kwa matakwa yake. Hii ni mali ya umma. kama kila mwenye pesa atakuwa na uwezo wa kulipia muda wa matangazo, si muda wote tutakuwa tunawaona watu wenye hela tu badala ya vipindi muhimu?? alihoji mwananchi mmoja katika mtandao wa kijamii.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana alisema kwa kifupi kuwa kipindi hicho ni sehemu ya vipindi vya kituo hicho cha televisheni.

Kile ni kipindi cha Chereko ambacho tunacho kwenye programu zetu,? alisema Mshana.

Alipoulizwa ilikuwaje ratiba ya kipindi hicho ikabadilishwa kutoka Jumapili mpaka Jumamosi, alisema: Kile ni kipindi cha wikiendi na kama mtu sherehe yake inafanyika siku hiyo, inakuwa haina shida yoyote.?

TBC ni shirika linalomilikiwa na Serikali likiwa na televisheni na redio.

Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, kituo hicho kilikuwa kikilalamikiwa kwa kuendesha kwa upendeleo kipindi cha Jambo Tanzania ambacho hupitia na kusoma magazeti makubwa ya kila siku. Katika moja ya vipindi hivyo, habari zilizokuwa zikihusu wagombea wa upinzani zilikuwa hazisomwi licha ya kuwamo kwenye magazeti yaliyokuwa yakichambuliwa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene amewahi kukaririwa akisema kuwa ameshaliandikia barua za onyo shirika hilo juu ya kukiuka kanuni za utangazaji ambazo hazitaki upendeleo wa aina yoyote
 
Dah hata mimi nimeona na imenisikitisha...... TBC nalo ni jipu kaka nape baba magufuli hebu litumbueni
 
Naangalia television ya Taifa muda huu nashaangaa kukuta harusi inarushwa live, inamaana television ya taifa haina kitu chochote cha kutuonyesha watanzania zaidi ya hiki kinachoendelea? Inasikitisha sana kwakweli

Halafu wengi wao wamesoma na wana digree na masters
Hata wenye elimu ya basic technician certificate wanawashinda
Hawana ubunifu hao, wanamavyeti tu ya kufaulu wakikariri basi
Nooo ubunifu.
 
Dah hata mimi nimeona na imenisikitisha...... TBC nalo ni jipu kaka nape baba magufuli hebu litumbueni

Mimi pia huwa nakerwa sanaa kwa TV ya taifa kurusha harusi, niliwahi kuwashauri kwenye banda lao saba saba kwamba kama wanapenda sana kurusha vipindi hivyo basi wafungue TBC starehe chanel just like EATV halafu huko warushe hayo maharusi, hata vigodoro wakipenda. Huku kwenye main station waweke vipindi vya maana.
 
Kwa TBC si ajabu! Hata nakumbuka wakati mwingine kuna maafa wao wakiendelea na taarabu! Tusubiri tuone kama watabadilika
 
Kama tumetaka chombo kijiendeshe kibiashara na kutengeneza faida, that means mwenye tukio anaweza akalipia na likarushwa live kama vile ambavyo wenye matukio mengine wanaweza wakalipia. Bila kutengeneza hela unadhani mishahara itapatikana wapi?
 
Naangalia television ya Taifa muda huu nashaangaa kukuta harusi inarushwa live, inamaana television ya taifa haina kitu chochote cha kutuonyesha watanzania zaidi ya hiki kinachoendelea? Inasikitisha sana kwakweli
TBC hii sasa ni zaidi ya Aibu hata kama ni biashara kwa upuuzi kama huu ipo siku watalipia kuchambana live
 
Hivi ikitokea HABARI MPASUKO hiyoo harusi yao itaendelea kurushwa ama... Sifa hazifai
 
Tatizo jamaa hao hawana ubunifu hata kidogo, mimi nafikiri hiyo inachangiwa na kupata ruzuku kutoka Serikalini - wachakalike wasichakalike mshahara wao hupo pale pale, sasa kuna haja gani ya kuwa wabunifu - yaani wasingeingia ubia na StarTimes sijui wangekuwa wageni wa nani - wanasikitisha sana. Bila ya JPM au Waziri mkuu kuifanyia mabadiriko/reform ya kweli kweli basi TV ya Taifa itapata wakati mgumu.Wekeni watu wabunifu na wenye uwezo mkiendelea kuweka watu kisiasa,kiushikaji na kujuana hamtafika mbali.
 
Hivi ikitokea HABARI MPASUKO hiyoo harusi yao itaendelea kurushwa ama... Sifa hazifai

Naona dalili kesho mheshimiwa rais kama anaona kinachoendelea hapa anaweza kuvunja bodi ya TBC. Hii Ni aibu kwa taifa
 
Back
Top Bottom