Wote tumeumbwa kwa sura na mfano wake Mungu. Hakuna ambaye ni mbaya. Hivi tulivyo ndivyo ilivyompendeza Mungu tuwe. Kukosoa kazi ya Muumba wetu ni dhambi.
Sent from my GT-N7100 using JamiiForums mobile app
Unatakiwa kufanyiwa maombi wewe pamoja na mumeo. Pepo la mauti linawawinda.Mungu akusamehe kwani hujui ulitendalo. Starehe ya muda inaweza kuwaletea maana wote wawili.
Sent from my SM-P601 using JamiiForums mobile app
Mbona hamuwaonei huruma vibaka mnawachoma moto hata wale walioiba kuku tu. Au suti walizovaa ndiyo zinazowafanya waonekane bora zaidi kuliko vibaka. Hao hawastahili staha, Mh Waziri Mkuu Big-Up Mungu atakulinda endeleza Mapambano wametutesa sana hao.
waambie hao Mwalimu Nyerere aliyeamulu wapigwe mboka 24 kwani alikuwa hajui kuwepo kwa haki za binadamu? watu wanafilisi uchumi wa Nchi halafu mnataka waonewe huruma badala ya kuonea huruma wagonjwa waliopo mahospitalini wanaopata shida kutokana na vitendo vya ufisadi vya wachache.
Wenyewe siyo wastaarabu kwa uzembe, wizi na Ufisadi wa mali za umma ambazo zi zetu sote wewe na mimi. Sasa unataka wafanyiwe ustaarabu gani zaidi ya kuwaumbua ili wajirekebishe na kutoa somo kwa wengine wenye tabia kama za kwao.
Acha kurudisha nyuma juhudi za Rais kutuletea maendeleo. Kama kuna matumizi ya hovyo ya fedha za vifaa vya usafi toa taarifa katika Taasisi zinazoshughulikia mambo hayo.
Hakika huyu si walewale. Huyu ni tofauti. Anajua wapi majipu yalipo na anaoutaalamu wa kuyatumbua. Ameomba jambo moja tu kwetu watanzania ili aweze kukamilisha kazi hii salama. Anaomba tumuombee ulinzi wa MUNGU. Natekeleza ombi lake nawe ufanye hivyo kwa faida ya Nchi yetu. MUNGU ibariki...
Nyie vipi! huyu pamoja na kuwa ni Rais wa Nchi pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa. Sasa kwanini asipigie debe chama chake? Kimshingi hili alishajibu kuwa chelekocheleko na mwenye mwana na yeye ndiye mwenye mwana wa mgombea wa CCM. Temeni kama vidonge alivyowapa vya uchungu.
Kupanga ni kuchagua. Hatuwezi kutekeleza yote ila tunaweka vipaumbele vya maendeleo yetu. Vipaumbele vinawekwa katika ilani kama chama chako hakina ilani hakifai na ni cha kukiogopa kama ukoma.
Si lazima apate kura yako. Ila wengine tutampigia kwa sifa alizonazo tunazozifahamu. Nina uhakika baada ya kampeni hata wewe utamkubali na utampigia kura kama una nia njema na Nchi yako
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.