Search results

  1. M

    Kujinasibu kwa wanasiasa kutoogopa kufa kunaakisi nini?

    Nimekuwa nikiwasikia wabunge kama Lema, Heche, Zitto, Bashe na wengine kadhaa wakijinasibu kuwa hawaogopi kufa! Nimekuwa nikijiuliza: hawaogopi kufa kwa ajili ya Taifa, nafasi na nafsi zao, au kwa kufahamu kuwa wanachofanya au kusema kina madhara kwao na taifa kwa kuwa ni kinyume cha sheria...
  2. M

    Ukosefu wa mafuta ya kula inaweza kuwa ni njama?

    Njama/hujuma mbalimbali kwa taifa, zinaweza kuangamiza nchi sawa na ramli chonganishi. Na mara nyingi hutokana na mapandikizi (watu) ya muda mrefu (kulingana na mikakati iliyokusudiwa) yaliyowekwa Serikalini au kwenye sekta za umma ili kuvuruga mfumo mzima unaohusiana na maisha ya wananchi ya...
  3. M

    Mchanganyiko wa tabia za mwanadamu hutokana na makuzi!

    Kiasili (nakubali kukosolewa), mwanadamu ameumbwa na mihimili: 1. Uvivu; 2. uchoyo na; 3. Ukatili. Pamoja na kuumbwa hivyo, bado mhimili wa tatu una mizizi mirefu na ndio huhinikiza na kuonesha tabia halisi ya mwanadamu (malezi) - chanya au hasi. Mhimili huu ukiwa na matokeo chanya ndio...
  4. M

    Ndani ya katiba mpya, Rais aondolewe kwa kura na sio kwa mihula miwili

    Kama katiba itatokea kufanyiwa marekebisho, nashauri raisi aondolewe na kura na sio kwa ukomo wa mihulai. Hii itamuwezesha raisi aliyepo madarakani kukamilisha dhima yake au kama ameshindwa, kumuondoa madarakani. Hali hii inaweza kumfanya kiongozi anayefaa kuendelea kuiongoza nchi na yule ambaye...
  5. M

    Najaribu kuwaza juu ya nani yuko nyuma ya uhalifu huu

    Watu kutekwa, kuuawa, kupigwa risasi, n.k. yanaonekana kuwa matukio ya kawaida na ambayo ukomo wake haujulikani utakuwa lini na kwamba, wahusika ni akina nani na wana maana gani! Najiuliza kwa sauti: 1. Je, ni serikali? Kama ni serikali, inafanya hivyo kwa sababu gani? 2. Je, ni vyama vya...
  6. M

    Wabunge wa CCM wanaoikosoa Serikali kinamna, kwa kutumia vyombo vya habari, kwanini wasitumie cocus yao?

    Kuna baadhi ya wabunge wa CCM ambao wamejenga utamaduni wa kuikosoa serikali kiaina kwa kutumia vyombo vya habari huku wakijua kuwa kuna caucus wabunge wa chama hicho ambayo inaweza kutumika vizuri bila kuonesha ufa wowote na serikali ikawaelewa vizuri zaidi. Kutumia vyombo vya habari kukosoa...
  7. M

    Usanii sadifu wa Mrisho Mpoto uundiwe tuzo au mtaala wa fasihi.

    Ndugu wagenzi wa fasihi, kama mlikuwa miongoni mwa waliotazama mazishi ya Marehemu Mzee wetu Kingunge Ngombale Mwiru, bila shaka Msanii mahiri wa ugani / tambo, Mrisho Mpoto aligusa nyoyo za waombolezaji na watazamaji wa mazishi yale kwa maneno mazito ya kizalendo na yenye hamasa kwa umoja na...
  8. M

    Ni kweli kwamba nchi yetu inahitaji ukombozi?

    Kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakijinasibu majukwaani kwamba wanataka kulikomboa taifa hili la Tanzania! Kwa kauli hizi nimekuwa nikijiuliza: hivi kumbe bado tuko kwenye ukoloni? Au labda wana maana kwamba CCM kukaa muda mrefu madarakani ni sawa na mkoloni? Sina uhakika kama neno hilo...
  9. M

    Bila kudhibiti uzazi, uchumi kukua itakuwa shida

    Wangwana, Nina wasiwasi kwamba, kasi ya idadi ya watu, ni sawa na kuchotea maji kwenye tenga. Sina uhakika kama wachumi waliomo kwenye mfumo wa utawala wanaliona hili. Na kama wanaliona, sina uhakika kama wanalitafakari na kulichukulia hatua sitahiki. Aidha, kwa wananchi wa kawaida, ambao ndio...
  10. M

    Hatima ya watoto wa mitaani kwa taifa letu ni nini?

    Wangwana wa JamiiForums, mara nyingi tumekuwa tukishuhudia Asasi za Haki za Binadamu zikikosoa serikali kwa masuala yasiyokuwa na tija kwa mustakabali wetu! Kuna suala la msingi sana la watoto wa mitaani /chokoraa ambao hawana makazi, hawajui watakula nini, hawajui msamiati wa elimu una maana...
Back
Top Bottom