Ndani ya katiba mpya, Rais aondolewe kwa kura na sio kwa mihula miwili

Massanda OMtima Massanda

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
1,056
561
Kama katiba itatokea kufanyiwa marekebisho, nashauri raisi aondolewe na kura na sio kwa ukomo wa mihulai. Hii itamuwezesha raisi aliyepo madarakani kukamilisha dhima yake au kama ameshindwa, kumuondoa madarakani. Hali hii inaweza kumfanya kiongozi anayefaa kuendelea kuiongoza nchi na yule ambaye hafai kuishia atakakoishia. Kura iamue na sio mihula!
Tuige mfano wa CHADEMA, Urusi, Ujerumani, Uchina, n.k
 
Huo utaratibu tayari upo , labda tu kwakua huelewi katiba, na watu kama nyie mpo wengi sana ambao hamuelewi lakini mnajifanya kuelewa sana na kuishia kupotosha wengine.
 
CHADEMA ni nchi gani?
 
Visiem hata ipitishwe katiba gani,hawa jamaa watashinda tu.wanaakili hadi zinawaletea uchizi
 
Kura zipi unazotaka coz Seif kapata kura nyingi na urais hakupata, Africa ili uwe rais sio kupata kura nyingi ni kujuwa kucheza game. nani hajuwi kuwa CCN hawapati kura halali bali haram za kibabe
 
Hoja yako ingekuwa na mashiko kama hakuna wizi wa kura na Chama dola wakati wa uchaguzi.
 
Huo utaratibu tayari upo , labda tu kwakua huelewi katiba, na watu kama nyie mpo wengi sana ambao hamuelewi lakini mnajifanya kuelewa sana na kuishia kupotosha wengine.
Hujamwelewa, anamaanisha kama Rais anakubalika aongoze hata mihula kumi....sio ukomo wa muhula miwili kwa katiba ya sasa
 
Kama katiba itatokea kufanyiwa marekebisho, nashauri raisi aondolewe na kura na sio kwa ukomo wa mihulai. Hii itamuwezesha raisi aliyepo madarakani kukamilisha dhima yake au kama ameshindwa, kumuondoa madarakani. Hali hii inaweza kumfanya kiongozi anayefaa kuendelea kuiongoza nchi na yule ambaye hafai kuishia atakakoishia. Kura iamue na sio mihula!
Tuige mfano wa CHADEMA, Urusi, Ujerumani, Uchina, n.k
aendelee kutawala ili aendelee kukuteua,uko sawa.
 
Ubovu ni kwamba rais aliyeko madarakani iwapo anahisi kwamba kura zitamkataa atashirikiana na chama chake kufanya hila ya kuchakachua hizo kura ili aendelee kuwepo.
Aliyepo sasa hivi anafanya yote ayawezayo kufanya yeye na chama chake waabudiwe kama Mungu!
Na waliomzunguka wata pambana kulinda nafasi zao
 
Hujamwelewa, anamaanisha kama Rais anakubalika aongoze hata mihula kumi....sio ukomo wa muhula miwili kwa katiba ya sasa
aliyeasisi huu mfumo alikaa ikulu miaka zaidi ya 20 na alijua kuwa rais anaweza kubaki ikulu hata kama raia hawamtaki ndiyo maana alikuja na mfumo wa miaka kumi ni muda unaotosha kutekeleza malengo na kumchosha kiongozi na kubaki ikulu kuwalinda wateule tu.
 
Kama katiba itatokea kufanyiwa marekebisho, nashauri raisi aondolewe na kura na sio kwa ukomo wa mihulai. Hii itamuwezesha raisi aliyepo madarakani kukamilisha dhima yake au kama ameshindwa, kumuondoa madarakani. Hali hii inaweza kumfanya kiongozi anayefaa kuendelea kuiongoza nchi na yule ambaye hafai kuishia atakakoishia. Kura iamue na sio mihula!
Tuige mfano wa CHADEMA, Urusi, Ujerumani, Uchina, n.k
Bado mpo tu watu mnaotaka kuondoa ukomo wa uraisi kwa mtindo wa mihula?
Acheni tabia za kichawi hizo.

Wazee walioweka ukomo wa miaka 10 waliweka kwa sababu za msingi na bado hizo sababu zingalipo na uhalali au uhalisia wake.
 
Na bado naamini zinatoa nafasi kuzibadilisha ili mradi utashi upo!
 
aliyeasisi huu mfumo alikaa ikulu miaka zaidi ya 20 na alijua kuwa rais anaweza kubaki ikulu hata kama raia hawamtaki ndiyo maana alikuja na mfumo wa miaka kumi ni muda unaotosha kutekeleza malengo na kumchosha kiongozi na kubaki ikulu kuwalinda wateule tu.
Je, yale mataifa niliyoyataja, pamoja na CHADEMA, mihula miwili haitoshi kutekeleza malengo yao? Ikumbukwe kwamba wakati mwingine ni nadra kumpata kiongozi mwenye uzalendo wa dhati wa kupigania maendeleo ya nchi. Mnapokuwa mmefanikiwa kumpata mtu wa namna hiyo, kura ziamue na sio mihula!
 
Huoni kwamba kiongozi mbovu anaweza kutengeneza mazingira ya kupata kura kwa hila ingawa kura hizo hazi akisi hali halisi ya utendaji wake?
Ukizingatia na elimu duni na uelewa mdogo wa wapiga kura wengi?

Mfano wako wa CHADEMA ni umejifunga hoja yako. Mbowe akianza vizuri lakini katiba yao ilipo ruhusu kuwa na tabia ya Mugabe na Museveni ndipo Mbowe akapata ujasiri wa kubadili gia angani sababu anajua atatumia ujanja na mabavu au mbinu chafu kubaki madarakani kwa vile katiba imempa mwanya huo.

Mbowe asingekuwa mwenyekiti 2015 nakuhakikishia Lowassa asingeruhusiwa kuiwakilusha CHADEMA uchaguzi mkuu wa 2015.
 
Nadhani mmoja ya kazi za Tume ya Uchaguzi na vyama vya siasa ni kuwapa wananchi elimu ya upigaji kura. Ni bahati mbaya kwamba vyama vya siasa vinajikita kwenye kulumbana badala ya kuwaonesha wananchi / wapiga kura ni kwa nini wao wanafikiri wakiwa madarakani watakidhi matarajio ya wananchi ili kwayo wananchi waamue ni nani wampe kura.
Aidha baadhi ya viongozi kuhama vyama vyao kunaashiria kwamba hata wao ama hawajui wafanyacho au wanajua walifanya makosa kuingia huko wanakotoka.
Kimsingi tukubaliane kwamba: "Katiba nzuri inatoa Tume ya Uchaguzi nzuri na Tume ya Uchaguzi nzuri inatoa viongozi wazuri (baada ya wananchi kuelemishwa vizuri juu ya namna nzuri ya kuchagua viongozi wao) na viongozi wazuri (kutokana na vyama kuwa makini juu ya kuteua wapigiwa kura) watatoa matokeo mazuri ambayo yataipeleka mbele nchi yetu kwa uzuri"
Bado nasimamia hoja yangu kwamba "raisi aendelee kuchaguliwa kwa kura, na sio kwa mihula"!
 
Back
Top Bottom