Kama kikokotoo kipya ni matokeo ya actuarial valuation ya mifuko, kosa la Irene Isaka ni lipi hadi atumbuliwe? Tusishangilie tuu...mwishowe...

Kama kikokotoo kipya ni matokeo ya actuarial valuation ya mifuko, kosa la Irene Isaka ni lipi hadi atumbuliwe? Tusishangilie tuu...mwishowe...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,042
Reaction score
132,825
1546149060214.png

Wanabodi
Jana nilibahatika kufuatilia mkutano wa Rais Magufuli uliofuta kikokotoo kipya na kurejesha cha zamani.

Taarifa ya Waziri Mhagama ilieleza uamuzi wa kikokotoo kipya ni kufuatia actuarial valuation ya afya ya mifuko iliyobaini mifuko ina hali mbaya ambapo kikokotoo cha 1:580
bado ni kile kile kwa sheria zote mbili ila tofauti ni malipo ya mkupuo kuendelea kulipa 50% kungeiua mifuko ya PSPS na LAPF hivyo ikaamuliwa malipo ya mkupuo yawe 25% kama ilivyo kwa PPF na NSSF ambayo malipo yao ya mkupuo ni 25% na sio 50% halafu ile 75% iwe distributed evenly for the rest of your life ambapo monthly pension inakuwa kubwa zaidi

Kiukweli kabisa nikisema sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana au sijui niite ni ujinga tuu, kuwahi kutokea duniani, wanashangilia kikokotoo kile kile na hakuna tofauti ya formula ya kikokotoo bado ni ile ile!. Irene Isaka ametangaza mbele ya rais jinsi kikokotoo kipya kitakavyo wafaidisha wastaafu in a long run, hiyo 50% ni hela nyingi but short lived!, hebu someni bandiko hili mshuhudie jinsi tulivyo wajinga
Kikokotoo cha mafao ya pensheni kilirekebishwa Julai 2014, na ndicho kinachotumika hadi sasa, japo jina la kanuni limebadilishwa.
pension_formula_2014-png.932966

Kikotoo cha pensheni cha mwaka 2014 (hapo juu) kilinganishe na kile cha mwaka 2018 (hapa chini)

pension_formula_2018-png.932967

Hivyo wajemeni, kikotoo bado ni kile kile cha 1:580

Swali langu ni bila kuingilia mamlaka ya rais ku hire and fire as he pleases, kama taarifa hiyo ya actuarial ni kweli, mifuko ina hali mbaya, kosa la Irene Isaka ni lipi hadi kupelekea kutumbuliwa?.

Hii ni kufuatia kila anayetumbuliwa kuonekana ni jipu mbele ya jamii, kuna uwezekano baadhi wanaotumbuliwa sio majipu bali ni kondoo tuu wa kafara?.

Wataam wa masuala ya pensheni tufafanulieni, kama taarifa ya Waziri Mhagama imesema hali ya mifuko ni mbaya, kikokotoo kingeendelea mifuko ingekufa, sasa rais amekirudisha, jee mifuko hiyo italipa pensheni hizo nene kwa uwezo upi, tusije kujikuta kwa sasa tunashangilia tuu halafu baadae tunakuja kukaza mikanda kwa government bail out kwa hazina yetu?.

Utumbuaji: Tuache Siasa Kwenye Professionalism, Sio Kila Mtumbuliwa ni Jipu!. - JamiiForums

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?! - JamiiForums

Hii Tumbua Tumbua ya Rais Magufuli, Hivi Kikwete Anajisikiaje?!. Anajisikia Sifa Au Anajuta?!. - JamiiForums

.
CB7F598C-F206-44C2-B4D2-EF819180D11B.jpeg
1546148811949.png
1546148887581.png

Jambo jingine la ajabu kuhusu pension ni ubaguzi wa wastaafu.
Jambo kubwa na la ajabu ambalo mimi kwa maoni yangu ninaona sio haki na sio fair, ni ubaguzi mkubwa wa mafao ya kustaafu kati ya viongozi wakuu na watumishi wa kawaida.

Mafao ya viongozi wakuu yanatawaliwa na Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1999, ambayo ilirekebishwa mwaka 2005, ambapo viongozi wastaafu wanalipwa pension kwa asilimia 80% ya mishahara ya walio madarakani, wakati wastaafu wengine wanalipwa mafao fixed kwa mujibu wa kikokotoo cha mfuko wa pesheni hisika.

Hii inawafanya viongozi wakuu kufaidika na kuongezeka pensheni mwaka hadi mwaka, wakati pensheni ya wastaafu wengine ni fixed!.

Wazazi wangu wote wawili, baba na mama ni wastaafu wa serikali. Baba tayari ni RIP lakini mama yupo na alistaafu mwaka 1990 akiwa ofisa wa juu wa serikali. Pension anayolipwa toka mwaka huo 1990 mpaka sasa is fixed, ukikisikia kiwango anachopokea, kiukweli, it's like a joke!.

Kwanini pension za viongozi wakubwa ziwe paged kwa percentage 80%, ya waliopo, lakini pension za wengine ni fixed kwenye kikokotoo cha mfuko ya pensheni?. Huu ni ubaguzi mbaya kabisa na sio kuwatendea haki wastaafu hawa!.

Utakuta mtu wa cheo cha Jenerali aliyestaafu 1990, analipwa pension ndogo kuliko Coplo au Sajent aliyestaafu 2015!. Is this fair?!.

And by the Way,
1546148850270.png

Ukimwangalia the way this lady look like, she looks like yule mama wa TIC aliyetumbuliwa, usikute...
it was just the most opportune moment to strike baada ya...
Kuna mambo mengine wajemeni yataka uwe na moyo haswa, sio mchezo...
hata ningekuwa mimi...
P
 
Wanabodi
Jana nilibahatika kufustilia mkutano wa Rais Magufuli uliofuta kikokotoo kipya na kurejesha cha zamani.

Taarifa ya Waziri Mhagama ilieleza uamuzi wa kikokotoo kipya ni kufuatia actuarial valuation ya afya ya mifuko iliyobaini mifuko ina hali mbaya ambapo kikokotoo cha 1:500 kingeiua mifuko ya PSPS na LAPF.

Bila kuingilia mamlaka ya rais ku hire and fire as he pleases, kama taarifa hiyo ya actuarial ni kweli, mifuko ina hali mbaya, kosa la Irene Isaka ni lipi hadi kupelekea kutumbuliwa?.

Hii ni kufuatia kila anayetumbuliwa kuonekana ni jipu mbele ya jamii, kuna uwezekano baadhi wanaotumbuliwa sio majipu bali ni kondoo tuu wa kafara?.

Wataam wa masuala ya pensheni tufafanulieni, kama taarifa ya Waziri Mhagama imesema hali ya mifuko ni mbaya, kikokotoo kingeendelea mifuko ingekufa, sasa rais amekirudisha, jee mifuko hiyo italipa pensheni hizo nene kwa uwezo upi, tusije kujikuta kwa sasa tunashangilia tuu halafu baadae tunakuja kukaza mikanda kwa government bail out kwa hazina yetu?.

P.
Ametumbuliwa kwa kushindwa kusimamia mifuko nafikiri unajua menejimenti za mifuko zilivyokuwa zinatumia pesa ovyo kwenye miradi ambayo haifai kama mradi wa Dege wa Kigamboni. Hivyo alisitahili kuachia ngazi ili wengine waongoze kwani yeye tu ndiyo anatakiwa kuongoza SSRA tangu 2012!!?
 
Hiyo vikokotoo vipya vianze kutumika kwa wanachama wapya na sio waliopo. Ni hatari kuanza kubadilisha rules of the game katikati ya game. Wakati najiunga umenambia nikistaafu nitalipwa hivi....nikakubali.....sasa iweje uanze kubadilisha mafao yangu bila ya kutaka ridhaa yangu kwanza?? Njia nyingine waweke utaratibu wa kujiunga au kujitoa kwenye hiyo mifuko kwa hiari....kama siridhiki na mafao yao iwe ruksa kujitoa na kupewa changu kwa wakati huo.
 
Huyu Mama Ni Mbuzi wa kafara
Ni Kama Dr Ibrahim Msabaha Kwenye sakata la Richmond 2007

Mswaada mpaka Kuwa Sheria unapita Kwenye Mikono, Taaasisi Na Mamlaka kadhaa

Kama Muswaada ule Mpaka Rais alisaini maana yake Kama Ni sifa ingesifiwa Serikal sasa iweje Kama Ni kosa alaumiwe Mtu mmoja personally?
Rais ana Mamlaka ya kutengua Muda wowote akijiskia lakin Kama katenguliwa Kwa kosa lile atakuwa kaonewa Sana
 
Kwani huyo bi dada aliwahi kueleza juu ya hali mbaya ya mifuko?
Je utaalamu wake ulimtaka awabambikie maumivu wastaafu au kusaka njia bora zaidi?

Kamwe hajawahi kusema kuwa mifuko ina hali mbaya..tena alishawahi kuwaambia mifuko hiyo kuwa wawe wanawalipa wastaafu bila longolongo yaani fasta bila usumbufu ila leo eti ni kondoo wa kafara
 
Wataam wa masuala ya pensheni tufafanulieni, kama taarifa ya Waziri Mhagama imesema hali ya mifuko ni mbaya, kikokotoo kingeendelea mifuko ingekufa, sasa rais amekirudisha, jee mifuko hiyo italipa pensheni hizo nene kwa uwezo upi, tusije kujikuta kwa sasa tunashangilia tuu halafu baadae tunakuja kukaza mikanda kwa government bail out kwa hazina yetu?.
Hakuna rocket sayansi hapa paskali,serikali ilipe trilioni 8 inazodaiwa na mifuko,hayo mambo mengine lissu anasema ni matango pori,hakuna mfuko utaofirisika kwa maana wanachama kila mwezi wanachangia mabilioni ya shilingi...

-Waachane na uwekezaji hewa kutapakanya fedha tu kama Dege village
-Kulipana mabonus hadi mili 400 hao wakurugenzi
-waache kukopesha wanasiasa
-wajikite kwenye miradi yenye tija tu tena itakayoidhinishwa na bunge.
 
SSRA imeshindwa kuisimamia mifuko, root cause ya tatizo sio mifuko kuwa na hali mbaya bali ni usimamizi mbovu wa fedha za mifuko uliopelekea mifuko kuwa na hali mbaya na kutaka kujikwamua kwa kuwaumiza wastaafu (wenye hizo fedha).
japo serikali (waziri na hata rais) hawawezi kukwepa lawama kwakua wao pia huchota fedha huko, juzijuzi tu hapa tulipokua tunaimba kama kasuku kuhusu 'serikali ya viwanda' kuna jiniazi mmoja alikua anaimuru hiyo mifuko ijenge viwanda, leo hii anajifanya hajui kitu.
 
Mifuko ilikuwa inakufa kweli. Ila kama ulimsikia Rais vizuri amesema yeye ataubeba huo msalaba kwa miaka minne hadi suluhu ya kudumu itapopatikana...
Huenda Irene ametumbuliwa kwa kufumbia macho miradi isiyo na tija kwa wanachama kama Dege eco village, na kushindwa kudhibiti high operational costs za mifuko mf kulipa kampuni ya ulinzi Tsh bilioni mbili!
 
Wanabodi
Jana nilibahatika kufustilia mkutano wa Rais Magufuli uliofuta kikokotoo kipya na kurejesha cha zamani.

Taarifa ya Waziri Mhagama ilieleza uamuzi wa kikokotoo kipya ni kufuatia actuarial valuation ya afya ya mifuko iliyobaini mifuko ina hali mbaya ambapo kikokotoo cha 1:500 kingeiua mifuko ya PSPS na LAPF.

Bila kuingilia mamlaka ya rais ku hire and fire as he pleases, kama taarifa hiyo ya actuarial ni kweli, mifuko ina hali mbaya, kosa la Irene Isaka ni lipi hadi kupelekea kutumbuliwa?.

Hii ni kufuatia kila anayetumbuliwa kuonekana ni jipu mbele ya jamii, kuna uwezekano baadhi wanaotumbuliwa sio majipu bali ni kondoo tuu wa kafara?.

Wataam wa masuala ya pensheni tufafanulieni, kama taarifa ya Waziri Mhagama imesema hali ya mifuko ni mbaya, kikokotoo kingeendelea mifuko ingekufa, sasa rais amekirudisha, jee mifuko hiyo italipa pensheni hizo nene kwa uwezo upi, tusije kujikuta kwa sasa tunashangilia tuu halafu baadae tunakuja kukaza mikanda kwa government bail out kwa hazina yetu?.

P.

Binafsi sioni kosa la Irene Isaka, lakini ndiyo hivyo tena...Dada huyu ni mchapa kazi wa ukweli na ameigeuza SSRA kuwa taasisi inayofanya kazi kwa weledi mkubwa utafikiri ni taasisi ya kimataifa...Kwangu mimi tatizo ni kuwa positions hizi huwindwa na watu wengi...majungu hayakosi...Lakini pia utendaji mbovu wa mifuko kama NSSF, PPF na hasa katika suala la uwekezaji nadhani ndiyo sababu ya watu wenye majungu..Binafsi sitashangaa kama akipata nafasi ya kimataifa..au pengine JPM anaweza kumpa kazi nyingine muhimu...Kwangu mimi kumuweka pembeni dada huyu ni kumpoteza mmoja wa wachapakazi wazuri ambao taifa hili limewahi kuwapata..
 
Wanabodi
Jana nilibahatika kufustilia mkutano wa Rais Magufuli uliofuta kikokotoo kipya na kurejesha cha zamani.

Taarifa ya Waziri Mhagama ilieleza uamuzi wa kikokotoo kipya ni kufuatia actuarial valuation ya afya ya mifuko iliyobaini mifuko ina hali mbaya ambapo kikokotoo cha 1:500 kingeiua mifuko ya PSPS na LAPF.

Bila kuingilia mamlaka ya rais ku hire and fire as he pleases, kama taarifa hiyo ya actuarial ni kweli, mifuko ina hali mbaya, kosa la Irene Isaka ni lipi hadi kupelekea kutumbuliwa?.

Hii ni kufuatia kila anayetumbuliwa kuonekana ni jipu mbele ya jamii, kuna uwezekano baadhi wanaotumbuliwa sio majipu bali ni kondoo tuu wa kafara?.

Wataam wa masuala ya pensheni tufafanulieni, kama taarifa ya Waziri Mhagama imesema hali ya mifuko ni mbaya, kikokotoo kingeendelea mifuko ingekufa, sasa rais amekirudisha, jee mifuko hiyo italipa pensheni hizo nene kwa uwezo upi, tusije kujikuta kwa sasa tunashangilia tuu halafu baadae tunakuja kukaza mikanda kwa government bail out kwa hazina yetu?.

P.
Fikiria, mtu anahama private kwenda serikalini, anaamua kuchukua pension yake yote huku akiwaambia rafiki zake kuwa kikokotoo kipya ni kibaya. Kingine yeye kama regulator alipaswa kufahamu/kushawishi umuhimu wa sheria mpya kuanza kutumika baadaye ili pawe na kipindi cha mpito. Huyu mama kosa lake ni kushindwa kumshauri rais/waziri, maana angesababisha watu kukosa imani na serikali na kupunguza ari na uzalendo wa kazi. Mi kwa upande wangu huyu mkurugenzi hafai kwa sababu huwezi kuongea academic kwa watu wa kawaida, hata waziri mhagama naye alikishwa sumu, maana unaposema mifuko mingine ilikuwa na uhai mpaka 2075 alimaanisha nini???
 
Back
Top Bottom