Mti wa Xmas wazua simanzi kwa wafanyakazi wa The Guardian Limited

Mti wa Xmas wazua simanzi kwa wafanyakazi wa The Guardian Limited

Sokoine

Member
Joined
Jan 26, 2011
Posts
34
Reaction score
55
Ni asubuhi na mapema. Wafanyakazi wa kampuni ya The Guardian Limited chini ya kampuni ya IPP wanaripoti kazini na kukutana na mti maridadi wa Christmas ukiwa na mapambo kwenye eneo la mapokezi.

Nyuma ya mti huo wa Krismasi kuna ukuta mweupe ukiwa na maneno makubwa The Guardian Limited -- The Home of Great Newspapers.

Kampuni ya The Guardian ni kampuni kongwe binafsi ya magazeti nchini ikichapisha magazeti pendwa kama The Guardian, Nipashe, The Guardian on Sunday, Nipashe Jumapili, Alasiri na mengine mengi.

Majonzi yanayowakuta wafanyakazi wa The Guardian Ltd kila asubuhi wakiingia ofisini na kuuona mti huo maridadi wa Krismasi ni simanzi waliyonayo baada ya kukaa miezi mitatu bila mshahara huku wakikosa kabisa matumaini ya kulipwa mshahara kabla ya Krismasi.

Hivi juzi tu kampuni hiyo imemaliza kuwalipa wafanyakazi wake mishahara ya mwezi Septemba 2018. Hii ina maana kuwa bado hawajalipwa mishahara ya miezi miwili -- Oktoba na Novemba 2018. Na huu Desemba sasa watatimiza miezi mitatu bila mshahara.

Kampuni ya The Guardian Limited inamilikiwa na mfanyabiashara mzawa Dk Reginald Mengi, ambaye kwa mujibu wa jarida la Forbes, ana utajiri wa zaidi ya dola za Marekani milioni 500. Licha ya utajiri mkubwa wa Dk Mengi, wafanyakazi wake wa The Guardian Limited wanaishi maisha duni bila mshahara kwa miezi mitatu.

Majuzi tu wafanyakazi hao wametoka kumzika mfanyakazi mwenzao mwenye ulemavu maarufu kwa jina la Bubu ambaye baada ya kukaa bila mshahara kwa zaidi ya miezi miwili na kunyimwa salary advance aliamua kupanda kwenye mnazi wa jirani yake kwa nia ya kuangua nazi ili apate hela. Matokeo yake Bubu huyo alidondoka kutoka juu ya mnazi na kuaga dunia.

Wakati Dk Mengi anafanya jitihada kubwa kuwekeza kwenye viwanda vipya vya dawa, simenti, magari, vifaa vya elektroniki na kubangua korosho, wafanyakazi wake wa The Guardian Limited wanakufa njaa.

Menejimenti ya The Guardian Ltd ambayo inaongozwa na raia wa kigeni kutoka India, wamekuwa wanamficha Dk Mengi ukweli kwani hana taarifa kuwa wafanyakazi wake wana miezi mitatu sasa bila mshahara.

Mtanzania aitwae Ayub Semvua ambaye ni mfanyakazi wa ITV/Radio One amekuwa anawasaidia raia hawa wageni kwa kuishi nchini kwa vibali vya kazi vya uongo kwa kutoa rushwa Idara ya Uhamiaji na Wizara ya Kazi.

Wageni hao ni:

1. S. Chintaluri, Meneja Mkuu wa The Guardian Limited
2. Murugan, Meneja Manunuzi
3. Bala, Meneja TeknoHama
4. Ajay - Director of Commerce (DC)
5. Balaji - Meneja uchapishaji

Wamedanganya wizara ya kazi kuwa hawa ni wakurugenzi wakati ni mameneja tu, kazi ambazo zinapaswa kufanywa na Watanzania.

Mbaya zaidi, hakuna vikao vyovyote vinavyofanywa na menejimenti kuongea na watumishi kuwajulisha mustakabali wa kampuni na kuwaeleza watalipwa lini malimbikizo yao ya mshahara wa miezi mitatu sasa.

Ni ajabu iliyoje The Guardian inaingia gharama kulipa wageni hawa watano Shilingi milioni 25 kila tarehe 23 ya kila mwezi wakati wafanyakazi wazawa wanakaa bila mshahara kwa miezi mitatu sasa.

Ewe mola, wasaidie wafanyakazi wa The Guardian Limited waondokane na simanzi, majonzi na masikitiko yao kila asubuhi waonapo mti huo wa Krismasi ofisini kwao, huku wakiwa hawana matumaini ya kulipwa mishahara yao ya miezi mitatu sasa kabla ya Krismasi.
 

Attachments

  • xmas.jpg
    xmas.jpg
    28.3 KB · Views: 170
Mkuu Sokoine, poleni sana!.
Mode naomba mlinde Sokoine, kitendo cha kutoa siri za kampuni humu, akijulikana atapoteza kazi.

Hii taarifa kuwa Kampuni ya Mzee Mengi inadaiwa, ni sawa na Mzee Mengi mwenyewe kudaiwa. Taarifa ya Mzee Mengi, ambaye ndiye tajiri mkubwa Tanzania, kudaiwa na wafanyakazi wake, sio taarifa mzuri kabisa, hivyo mimi nakubaliana na mtoa mada kuwa Mzee Mengi mwenyewe hajui kuwa wafanyakazi wake wa the Guardian Ltd, hawajalipwa mishahara ya miezi mitatu, hivyo kwa taarifa hii sasa, habari ndio zitamfikia, atachota akiba yake na kulipa hiyo mshahara, kati ya kesho na Ijumaa watalipwa.

Poleni sana
P.
 
Poleni, kampuni nyingi zinayumba kibiashara ktk awamu hii ya 5 ya CCM . Fanyeni maamuzi magumu Oktoba 2020 muache mazoea ya kuirudisha CCM madarakani.

Wafanyakazi wanashindwa kuitofautisha kampuni na Reginald Mengi. Kisheria kampuni na Mzee Mengi ni 'watu wawili tofauti ' , ndo maana utaona kampuni inashitakiwa pekee bila Mzee Mengi kujumuishwa.
Kwa mujibu wa Advocate Jebra Kambole Mtaalamu wa Sheria anayefanyia kazi katika Kampuni ya Law Guards Advocates, ya Jijini Dar es Salaam ktk Makala yake maalum ndani ya gazeti la Mwananchi: Kampuni ni mtu kisheria (Artificial person) tofauti na wanahisa au wanachama wake, ina uwezo wa kushitaki na kushitakiwa : bofya / click hapa usome makala nzima ya gazeti la Mwananchi : Jinsi ya kuwa na kampuni binafsi .

Wafanyakazi wa the Guardian labda mseme mnataka zawadi toka mfukoni na siyo ktk mshahara wenu toka fuko la kampuni tutawaelewa.

Ila mtambue Utajiri unaozungumziwa ktk jarida la Forbes, mwingi ni assets yaani uwekezaji wa vitu halisi na siyo cash ktk akaunti binafsi iliyopo benki.
 
Mkuu Sokoine, poleni sana!.
Mode naomba mlinde Sokoine, kitendo cha kutoa siri za kampuni humu, akijulikana atapoteza kazi.

Hii taarifa kuwa Kampuni ya Mzee Mengi inadaiwa, ni sawa na Mengi kudaiwa. Taarifa ya Mengi kudaiwa sio taarifa mzuri, mimi nakubaliana na mtoa mada kuwa Mzee Mengi hajui kuwa anadaiwa mishahara ya miezi mitatu na wafanyakazi wake, hivyo sasa mshahara utashughulikiwa kesho na utalipwa Ijumaa.

Poleni sana
P.
Anrhony Dialo kule star media nadhani wafanyakazi wameamuwa kujitolea tu, walishasahau kitu kinaitwa mshahara.
 
Back
Top Bottom