Baada ya Serikali kusema ipo tayari kulipia matibabu ya Lissu; Peter Msigwa, Godbless Lema na Mbowe wakosoa kauli hiyo

Baada ya Serikali kusema ipo tayari kulipia matibabu ya Lissu; Peter Msigwa, Godbless Lema na Mbowe wakosoa kauli hiyo

Ujinga pia ni kutokufuata utaratibu wa bunge wa kimatibabu kisha kuwachangisha wananchi wanyonge hela ya matibabu.
Rais na Serikali vinajaribu sana kuaminisha Taifa kuwa aliye na "maisha mazuri" Ni Shetani, Ni mwizi, Ni fisadi! Si kweli na si sahihi!
 
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kutoa kauli yake baada ya serikali kusema ipo tayari kulipia gharama za matibabu ya Tundu Lissu popote duniani na kusema huo ni utani wa serikali ya awamu ya tano.

Mbunge Msigwa ametoa kauli hiyo baada ya masaa kadhaa kupita toka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kusema kuwa serikali ipo tayari kulipia gharama za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu popote duniani baada ya kupata maombi kutoka kwa familia ya Tundu Lissu na kama ripoti ya madaktari itaonyesha kuna ulazima kiongozi huyo kupatiwa matibabu zaidi basi serikali itasimamia jambo hilo.

Kutokana na kauli hiyo Msigwa amedai huo ni utani wa serikali "Huu ni utani wa serikali ya awamu ya tano" alisema Peter Msigwa

Mbali na hilo Mbunge Peter Msigwa jana alisema kuwa wao wanatambua thamani na umuhimu wa Tundu Lissu na kusema kuwa wapo tayari kuuza vitu vyao mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anapata matibabu na kurejea nchini akiwa salama.
=============================================================================

Nae Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alikuwa na haya ya kusema


Kwa ufupi;
Asema nashangazwa sana na taarifa alizotoa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ya kwamba familia ya Lissu iandike barua kama wanahitaji matibabu na kwamba serikali ipo teyari kumtibu Mhe. Lissu mahali popote duniani.

Amemtaka Waziri huyo aache uongo na upotoshaji serikali haipo teyari kumtibu Lissu mahali popote Duniani ndio maana Spika kwa Kinywa chake alikataa ana akasisitiza kwamba wao wasingeweza kumtibu Lissu katika hospitali ya Nairobi ambapo sisi tuliamini kuwa kulikuwa na vifaa vya kuweza kuokoa uhai wake.

Pia amesema hakuna utaratibu wa kibunge ambapo mbunge anapokuwa mgonjwa kwamba familia yake ndio inaandika barua na kuelezea bunge kuwa huyu ni mbunge na anahitaji msaada wa kibunge. Bunge lina Katibu na Spika, Spika alikuwepo wakati Lissu anasafirisha anajua Lissu alipo lakini hajachua utaratibu wowote.

Amesema leo ni siku ya 14 lakini si Spika wa naibu wake wala Katibu wa mtu yeyote kutoka katika sekretariet ya bunge aliyewahi kurusha mguu kuja kujua anaendeleaje
============================================================================

Nae Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni na Mbuge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe akihojiwa na Sauti ya America jioni hii, alikuwa na haya ya kusema;

Kiongozi wa kambi rasmi ya upunzani bungeni na Mbuge wa hai Freeman Mbowe amekosoa vikali kauli ya serikali kuhusu utayari wa serikali kugharimia matibabu ya Lissu popote duniani.

Mbowe akihojiwa na Sauti ya America Washington, amekaririwa akiilamuu serikali kwamba imekaa kimya tangu jaribio la kumuua Tundu Lissu mpaka leo takribani wiki 2. Amenda mbali zaidi kwa kuhoji iweje serikali isubiri maombi kutoka familia ya Lissu ikiwa utaratibu wa matibabu ya Mbunge ndani na nje ya nchi yanashughulikiwa na bunge moja kwa moja kupitia kamati za bunge na kwamba hakuna mbunge aliewahi kupitia utaratibu huo.

Mahojiano zaidi ya Mhe Freeman Mbowe sikiliza hapa; Mhe. Mbowe akihojiwa na Sauti ya America.mp3
============================================================================

" Swali la Kizushi: WATU WASIOJULIKANA NI WALE WALIOKUJA KUTOKEA ILE NCHI JIRANI KUFANYA ILE SHUGULI?

Iweje wauuaji ndiio wagharimie matibabu? Bashite anatakiwa kuwa mahabusu wakati ucchunguzi ukiendelea
 
Familia ndiyo yenye uchungu mkubwa kuhusu maisha ya ndugu yao Kibaraka Lissu. Nyie kina Mbowe hamjui umuhimu wa Kibaraka Lissu zaidi ya ule msaada anaotoa kwenye chama chenu hamjui ana umuhimu gani kwenye familia yake. Mmempeleka Nairobi Kibaraka Lissu, lakini mkiwa na agenda zenu...mmekwenda Nairobi kisiasa, hata mimi ningelikuwa mwanafamilia ningeliomba msaada kwa serikali. Hali ni tete, Watanzania tumechoka kutembezewa bakuli la michango wakati njia ya matibabu kwa kodi zetu wenyewe iliwezekana kuhudumia Kibaraka Lissu kupitia serikalini ila nyie kwa maslahi yenu ya siasa mkaleta siasa. Sasa familia imewageuka...
 
Wangewacha wacha hizi siasa za ushindani na wakawashauri familia ya Lissu wapeleke hayo maombi, Tuombe ukweli kama yangetimizwa.

Au kuna wa zile tuhuma za nia ya ufujaji wa zile pesa?

Maana Serekali kutimiza dhamira yake ya kumtibu lissu popote duniani, basi kuna wengi wTakosa kula
 
Wa Tz nani katuloga kama serekari imekubali kusaidia matibabu Ls litakuwa jambo jema tulipokee tunachohitaji sisi ni kuona Ls analejea katika hari yake na si vinginevyo tusitengeneze kauli zitakazo wafanya serekari kughaili jambo hili kwa kauli zetu
Iweje mchawi amtibu mwanao aliyemloga yeye?
 
cc: Abdallahkova.
Soma kwenye maandishi mekundu hayo. Halafu potea na UONGO wako.
Pathetic Swine.
9dcf3e407b22e8b4ad55e8753c6bbd78.jpg
soma vizuri hapa .
 
Tumia Akili wewe
Familia Iliingizwa kwenye Siasa na kuona kama serikali inahusika kwa tukio hilo
wakaona bora wakomae wenyewe
leo uamue kumtibu kwanguvu na ikatokea Akafariki
unadhani familia itaacha kuamini Upuuzi wao kuwq Serikali inahusika!!
Hata kama ninyi nivibendera mjaribu kuangalia kidogo kuna muda upepo unatulia kibendera hakifuati Kitu!!
Hadi mwisho wa dunia familia itaamini hivyo. Hata serikali ifanye nini hawatabadilisha mawazo. Kumbe serikali inajisafisha isionekane imehusika. Tukio lilivyotokea serikali haikuwepo.
By rhe way familia haina shida ya kuomba serikali imjibu. Sheria taratibu na miongozo ipo wazi kabisa kuhusiana na matibabu ya mbunge. Watanzania wenye mapenzi mema bado wanaendelea kuchanga kwa kasi sana. Kama umetumwa kawaambie nimekuta wapo macho
 
Watanzania kama comments utazipata vizuri ila kutoa pesa weeeee! kama nilielewa vizuri walisema Familia ndio iliomba akatibiwe kenya .Inshort haikuwa na imani na serikali sasa leo mnaposhindwa kulipa kwanini msirudi tena kwa serikali ile ile ambayo hamna imani nayo mnaitusi kwenye tv ili iwasaidie gharama.
 
Wekeni akiba ya maneno.
Hamkumbuki familia ilikataa kufuata utaratibu wa kawaida ya Kutibu wabunge.sasa mbowe ulitaka walazimishe au wanyanganye mgonjwa?
Na familia haijaomba msaada. Watanzania wenye mapenzi mema na walioumizwa na hilo tukio watachanga. Leo imemtokea yeye kesho inamtokea ndugu yako au wewe mwenyewe.
 
Ulisikia wapi mwananchi kutibiwa na serikali yake anayo ilipa kodi ni mpaka familia yake iombe? Huo sio utaani?
Ummy ni mrembo sana, hastahili kufanya kazi na hii mijamaa yenye roho mbaya sema ndo hivyo tena! Huyu angekuwa nchi iliyostaarabika kama USA alistahili kupewa umakamu First Lady!
 
Upinzani wa Tanzania bwana ni vichekesho kabisa, wakikamia kitu mpaka Basi, ni kwel tunatakiwa kuhoji na kjadili suala la matibabu ya Lissu. Ila mjue kwamba pamoja na hilo population ya watu Ml 49 wanaendelea na maisha ya kila siku kama kawaida, nikimanisha bado kuna watu wana shida kama au zaidi ya hyo wanahitaji msaada wenu wa khali na mali, tusijifanye kwamba shughuli zote za kumtetea mtanzania ziko kwenye kujadili suala la kuokoa maisha ya mtu mmoja tu wakati wengine wanapoteza maisha. Kwa hyo bas ni ushaur wangu kwamba tuendelee na kujadili masuala ya Lissu pamoja na wananchi wengine wanaoitaji msaada kama ilivyo kwa Lissu tofaut na hapo tutakuwa tupo kisiasa zaidi wala sio kumtetea mwananchi mnyonge
 
Wee acha kiburi chao kitawacost .Bili ikifika Bilioni moja ndio watajuta na ujinga wao . unashindana na serikali wewe unatoa mitusi alafu unaomba ukatibiwe . wengine tuna matatizo lukuku Tundu ni nn ? msituzingue manyumbu

Kwani na hiyo unayoita serikali ni nini? Nani kaomba atibiwe na serikali?
 
Ee Mwenyezi Mungu naomba uzidi kuimarisha afya ya Lissu na uponyaji wa haraka. Amen
kila moyo wenye nia njema na afya ya LISSU umesema AAAMEN! sala fupi ila imenigusa moyoni., na MUNGU, JEHOVAH, ALLAH, EBENEZA; vyovyote unavyomutaga, amesikia sala yako na muujiza unaendelea kutendeka
 
Back
Top Bottom