Rais Magufuli azindua barabara ya KIA hadi mji wa Mererani, Awataka JWTZ kujenga Ukuta kuzunguka Machimbo ya Tanzanite

Rais Magufuli azindua barabara ya KIA hadi mji wa Mererani, Awataka JWTZ kujenga Ukuta kuzunguka Machimbo ya Tanzanite

Umeona vijembe vya Trump dhidi ya North Korea na Iran?Hiyo ndiyo mipango ya maana? UN hakuna lolote,ni kijiwe cha wahuni tu, waabudu Shetani.
kama ni kijiwe cha wahuni na waabudu shetani magufuli kamtuma mahiga kufanya nini huko new york?
 
Ni wakati muafaka kwa raisi wetu mpendwa kuhudhuria mikutano ya kimataifa na kuimarisha/ kutengeneza connections na marais wa nchi mbalimbali..hili suala la kujifungia kwa maoni yangu naona kama haliwezi kuwa na msaada mkubwa kwetu kama taifa ukizingatia tuko katika kipindi ambacho mabeberu wengi wanatuzonga kisa tumewabania njia zao za kuiba rasilimali zetu za asili. Kuzindua barabara ibakie kuwa ni kazi ya waziri ama mkuu wa mkoa. Please naomba msinitumie nissan nyeupe ni ushauri tu wa bure[emoji38][emoji38]
 
Means hukupaswa kuandika lawama usizota kutolea maelezo na wewe nu mmoja wa spin dr na waotoshaji wenye lengi la kudhoofisha juhudi za serikali kuinua uchumi kwa kutumia Rasilimali zetu.
Mtu mzima km wewe unapotosha na kutaka Watanzania waamini Natural Resources haziwezi kuinua uchumi wa Taifa? Acheni upuuzi wenu huu
You won't understand now ..... when we talk about the global you think we are talking about the earth. That's the difference!!
 
There is nothing tangible kwenye kifaa cha wamarekani kulazimisha matakwa yao ya kisiasa, kidiplomasia na kiuchumi tena kwa ubabe!! UNGA ni tool ya US. Ebu rejea hotuba ya ovyo ya yule 'mumsujudiaye ' kwa ubora wa demokrasia
Wenzake wako UN huko kupanga mipango ya maana yeye kazi kutafuta majukwaa ya kupiga vijembe wapinzani. Watanzania tumekula hasara kwa miaka mitano.
 
Wenzake wako UN huko kupanga mipango ya maana yeye kazi kutafuta majukwaa ya kupiga vijembe wapinzani. Watanzania tumekula hasara kwa miaka mitano.
Tupo tayari kula hasara na miaka mitano ijayo ila sio kumkubali mamvi wenu
 
Hongera kwake Rais Magufuli. Mungu akitujalia tukapata Marais kama Magufuli kwa Miongo mitatu mfulizo Nchi hii itapiga hatua kubwa sana.

Ila tukae tukijua Mataifa ya magharibi hawapendi kabisa Taifa la kinyonge lielekee kujikomboa na kiuchumi na kujitegemea katika nyanja zote.

Tuungane na Rais Magufuli bila kujali makundi yetu mbalimbali tuweke Utanzania mbele.
 
Tukishaweka uzio tuwapige risasi watakaojaribu kutorosha, vita lazima vipiganwe kwa bunduki na risasi hata kama ni vya kiuchumi,

pia kuweke viwango vya kuuza madini yetu sio kusombwa kiholela tu, wachimbe miezi mitatu tu kwa mwaka.
 
Wenzake wako UN huko kupanga mipango ya maana yeye kazi kutafuta majukwaa ya kupiga vijembe wapinzani. Watanzania tumekula hasara kwa miaka mitano.
Huko UN ni nyumbani kwako wewe vip? shughulika na nyumbani kwanza, wewe huko Un hawagawi fedha wewe ama ulimzoea yule ombaomba? Hongera Magu
 


Habari waungwana,
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameshatua uwanja wa ndege wa Kilimanjaro na kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Elisha Mngwira. Muda mchache ujao anatarajiwa kuzindua barabara ya KIA mpaka Mererani.

Fuatana nami kujua yanayojiri..
====

Magufuli: Adui yetu mkubwa ni maendeleo sio vyama, ninawashukuru sana kwa kura, nina uhakika hata Malya alinipa, nawashukuru sana wizara ya ujenzi na uchukuzi, TANROADS, wakandarasi na consultants ambao wamefanikiwa kumaliza hii barabara hii ya KM 26 kwa gharama ya bilioni 32.5 na fedha zote zimetokana na kodi za watanzania, nawapongeza sana watanzania wanaolipa kodi.

Barabara ambazo tumeamua kutengeneza zipo yingi, tumeanza na Km 26 lakini haiwezi kuishia hapa kabla haijafika makao makuu ya wilaya na Mkoa.

Nawapongeza sana kwa kumchagua Milya, amelelewa na CCM. Nchi hii ni tajiri na historia inazungumza wazi, tukapewa madini ambayo hayapo pengine kokote duniani, tujiulize haya madini yanatusaidia? Mungu ametupa madini lakini tunapata shida ndio maana nimefika hapa ila mtu analilia shida, Tanzanite tunayo lakini tunaitumiaje? Tulimkosea nini Mungu? Hilo ndio somo langu la leo.

Tanzania matatizo yetu sio vyama, matatizo yetu ni kwanini tunaibiwa? Wangepewa nchi nyingine, hapa pangekuwa kama Ulaya. Ripoi ya Tanzanite iliyoundwa na Spika, Tanzania haiwanufaishi hata wananchi wa hapa, pia haiwanufaishi watanazania. Tanzania inapata asilimia tano, ndio maana nasema nasema tuna changamoto.

Katika uongozi wangu nimeamua kuongoza hii vita, naomba tusimame pamoja kushinda hii vita. Tanzanite ina eneo la kilometa za mraba 81.99, kuna block zimegawanywa. Tanzanite zinaibiwa sana, ni shamba la bibi, nafikiri mabibi waliokufa miaka mingi sana.

Kuna wawekezaji ambao wana asilimia 50 lakini mali zinasombwa. Nimeamua lile eneo ili tuzuie wizi, block A mpaka D, naagiza JWTZ waanze kulijenga ukuta eneo lote, kazi ifanyike haraka. Wakimaliza wake fence na kamera, kutakuwa na mlango mmoja. Hata kama utameza Tanzanite itaonekana.

Serikali ipate pesa yake na mchimbaji apate pesa yake, tunataka soko la Tanzanite liwe hapa Simanjiro na wala sio Arusha. Wanunuzi wote waje kununua hapa Simanjiro, barabara ni lami.

Nimeona tuanze na hii hatua, nina hakika watu wa Tanzanite one na wengine watakaa na kutengeza mkataba wenye faida kwa serikali. Ni lazima tujipange vizuri, hili suala naona sasa linafika mwisho wake.

Biashara haijazuiliwa lakini tunaitoa kwenye biashara ya magendo kuwa biashara halali. Ukishapata mali yako ndani ya uzio, peleka kwenye duka lolote na wateja watakufata hapo hapo. Biashara hii unaondoka umeficha na unapeleka anakulalia kwa sababu anajua huwezi kuipeleka popote.

Benki kuu pia watengeze mkakati wa kushiriki katika kununua zawadi. Tuna madini kila maali lakini majamaa wamekuwa wakisomba tu, tunaendelea kubaki maskini.

Nafahamu katika hatua mlizoanza kuchukua, kuna wengine wamekimbia na hamtawaona kwa sababu ya waliochokuwa wanafanya.

Malya sio adui yetu, adui yetu ni yule anae tuibia. Barabara imejengwa na CCM lakini watapita watanzania wote, tunagombania nini? Wanasema kitunze kidumu, naomba mtunze hii barabara. Kuhusu suala la maji naomba mniachie, kuna mradi mkubwa wa bilioni 45 kwenda makao makuu ya wilaya, eneo hili ambalo halina vyanzo vya maji naomba mniachie.


SINA UHAKIKA KAMA BARABARA IMEJENGWA NA CCM, NINACHOFAHAMU BARABARA HUJENGWA KWA KODI ZA WANANCHI WALA SI KWA MICHANGO YA KADI ZA CCM ZA TSH 1500.
 
Wenzake wako UN huko kupanga mipango ya maana yeye kazi kutafuta majukwaa ya kupiga vijembe wapinzani. Watanzania tumekula hasara kwa miaka mitano.
Huko UN tunapata nini? Anachofanya rais ni kutekeleza siasa ya self reliance aliyoanzisha Mwl Nyerere.
 
Kweli adui yetu mkubwa ni maendeleo, ndio maana twarudi nyuma.
 
Back
Top Bottom