Rais Magufuli azindua barabara ya KIA hadi mji wa Mererani, Awataka JWTZ kujenga Ukuta kuzunguka Machimbo ya Tanzanite

Rais Magufuli azindua barabara ya KIA hadi mji wa Mererani, Awataka JWTZ kujenga Ukuta kuzunguka Machimbo ya Tanzanite

Huku mtaani habari ni Lissu tu, raia hawajui hata kama tunaye Rais nchi hii
 
Tangu saa kumi na mbili watu wamekaa chini wanasubiri Rais afike,naona jukwaa liko vizuri lakini uwanja ni mdogo sana
 
Mhesh Rais Magufuli ameagiza JWTZ kuanza ujenzi wa ukuta kuzunguka maeneo ya machimbo ya Tanzanite maramoja.
Aidha ameagiza kuwa soko la tanzanite lijengwe Simanjiro.
Pia ameagiza kupitia upya kwa mkataba wa uchimbaji madini kupitia kamati maalumu ya Professor Kabudi. Mkataba ya unyonyaji ikome.
Wachimbaji wadogo wataruhusiwa kuchimba tanzanite na kuuza madini hayo ndani ya soko litakalojengwa ndani ya uzio huo.
Ameagiza BOT kuandaa mkakati wa ununuzi wa madini hayo.
Ameahidi kuwaletea Ambulance wakazi hao wa Mererani.
Wawekezaji wanakaribishwa ila sio wanyonyaji.
Watanzania wameombwa kusimamia rasilimali zao vizuri.
Mhesh Rais amesema adui wetu niwale wanaotuibia rasilimali zetu hivyo tushikamane wote.
Mhesh. Rais Magufuli amewaomba wananchi hao wamuachie tatizo la maji atalishughulikia.
Mhesh Rais pia amesema Tanzania haikuumbwa kwa ajili ya mafisadi bali watanzania masikini na wanyonge,ameahidi kulala nao mbele watu hao.
Viongozi wameagizwa kukaa pamoja na kutatua kero wananchi.
Wana CCM watakaoomba nafasi za uongozi kwa kutumia bongo wasichaguliwe na pia hats huko juu hawatapitishwa.
Amemaliza na sasa anajiandaa kufungua rasmi barabara husika.
 
Wananchi wanalalamika na raisi analalamika.
 
Magufuli: "Adui yetu mkubwa ni maendeleo sio vyama"

Hapa kachapia au kamaanisha?

Mbona kazi?
 
Back
Top Bottom