Serikali yakanusha kuhusu likizo isiyo na Malipo kwa Wanaoenda Kusoma

Serikali yakanusha kuhusu likizo isiyo na Malipo kwa Wanaoenda Kusoma

Mbona sasa hakuna kilichokanushwa hapo haki Mungu namba tutaendelea kusoma tu. Nilikuwa natamani sana nikasome lakin sasa basi hakuna namna tena.
 
Msaada ta
Hili suala mbona lipo bayana siku zote hawa wanaosambaza tarifa kama hizi wehu kitu kiko bayana kabisa siku zote.
Msaada tafadhali. Hili tangazo linahusisha idara zote? Kuna academicians na researchers wako masomoni na wanalipwa, je utaratibu huu utawaathiri pia?
 
Tahadhari:

Kumekuwepo na taarifa ya upotoshaji ikisambazwa kuonyesha kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais- Utumishi wa Umma na Utawala Bora amefuta yafuatayo:

1. Malipo ya uhamisho kwa anayehama kituo cha kazi bila ya kuhama Wilaya au Mkoa anaofanyia kazi. Mathalani, Mwalimu anayehamishiwa kutoka Mbagala kwenda Temeke hawezi kulipwa malipo ya uhamisho.

2. Likizo yenye malipo kwa wafanyakazi wanaokwenda masomoni kuchukua shahada ya kwanza

3. Likizo yenye malipo kwa wafanyakazi wanaokwenda kusomea shahada ya uzamili na elimu ya juu.

Ukweli ni kuwa haya yote si mambo mapya na yako katika Standing Order. Tokea awali, Mfanyakazi anayekwenda kusomea shahada ya kwanza hupewa kibali na likizo bila malipo.

Kwa upande wa shahada ya uzamili na uzamivu, Kanuni G7 2 (a) na (b) (i)na (ii) inaeleza bayana kuwa:

1. Kanuni ya G2(b)(i)Ikiwa atakwenda kusomea shahada ya uzamivu na uzamili atapewa likizo yenye malipo iwapo anachokwenda kusomea kiko katika mpango wa maendeleo ya rasilimali watu wa Wizara.

2. Kanuni ya G2 (b)(ii) Atachukua likizo bila malipo hata kama anakwenda kusomea Shahada ya Uzamili na Uzamivu kama anachokwenda kusomea hakiko kwenye mpango wa Wizara yake wa Maendeleo ya Rasilimali Watu alimradi awe amemaliza miaka 2 ya utumishi tokea alipoajiriwa.

Utumishi wa umma daima huongozwa kwa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ambayo hutolewa kupitia waraka mbalimbali. Ndio kusema kuwa katika hili linalosambazwa, hakuna taarifa mpya. Jiridhishe na nakala za Kanuni hapa chini.
Mambo haya yapo ki sheria kanuni na utaratibu iweje mnaruhusu upotoshaji na mbaya zaidi habari zinatolewa kiholela kwenye social media kwa nyaraka toka kwa wakuu wa idara baadhi ya Halmashauri. Hivi wao ni akina nani wanaopotosha na kuleta taharuki kwa watumishi wa umma.
 
Kumbe ni kuwa hawa wasambaza taarifa walichokifanya ni kuwazindua tu watu ambao hawakuwa na habari hizi. Na mi nmeelewa hili. Noted!!
 
Tahadhari:

Kumekuwepo na taarifa ya upotoshaji ikisambazwa kuonyesha kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais- Utumishi wa Umma na Utawala Bora amefuta yafuatayo:

1. Malipo ya uhamisho kwa anayehama kituo cha kazi bila ya kuhama Wilaya au Mkoa anaofanyia kazi. Mathalani, Mwalimu anayehamishiwa kutoka Mbagala kwenda Temeke hawezi kulipwa malipo ya uhamisho.

2. Likizo yenye malipo kwa wafanyakazi wanaokwenda masomoni kuchukua shahada ya kwanza

3. Likizo yenye malipo kwa wafanyakazi wanaokwenda kusomea shahada ya uzamili na elimu ya juu.

Ukweli ni kuwa haya yote si mambo mapya na yako katika Standing Order. Tokea awali, Mfanyakazi anayekwenda kusomea shahada ya kwanza hupewa kibali na likizo bila malipo.

Kwa upande wa shahada ya uzamili na uzamivu, Kanuni G7 2 (a) na (b) (i)na (ii) inaeleza bayana kuwa:

1. Kanuni ya G2(b)(i)Ikiwa atakwenda kusomea shahada ya uzamivu na uzamili atapewa likizo yenye malipo iwapo anachokwenda kusomea kiko katika mpango wa maendeleo ya rasilimali watu wa Wizara.

2. Kanuni ya G2 (b)(ii) Atachukua likizo bila malipo hata kama anakwenda kusomea Shahada ya Uzamili na Uzamivu kama anachokwenda kusomea hakiko kwenye mpango wa Wizara yake wa Maendeleo ya Rasilimali Watu alimradi awe amemaliza miaka 2 ya utumishi tokea alipoajiriwa.

Utumishi wa umma daima huongozwa kwa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ambayo hutolewa kupitia waraka mbalimbali. Ndio kusema kuwa katika hili linalosambazwa, hakuna taarifa mpya. Jiridhishe na nakala za Kanuni hapa chini.
Mkuu, umetuambia tujiridhishe kwa kupitia nakala ya Kanuni hapo chini, mbona hukuattach hiyo nakala ya Kanuni??

Pili, Umenukuu Kanuni G 7 2 (a) (b) (i) na (ii) kwenye Standing orders, mbona standing orders of 2009 haina Kanuni G7 2(a) (b) (i) na (ii)??? Umetumia standing orders ya mwaka gani??

Tatu, Umenukuu Kanuni G 2(b)(i) na G 2(b) (ii) kuwa zinazungumzia maswala ya likizo za masomo ya Shahada ya uzamivu na uzamili, Mbona standing orders ya 2009 haina Kanuni G 2(b)(i)na (ii) na badala yake Ina Kanuni G.2 ambayo haizungumzii mambo uliyoyaeleza hapa??

Mwisho, maelezo haya na hizi Kanuni umetoa wapi?? Tafadhali weka hiyo nakala ya Kanuni uliyoahidi kuiweka!!

Asante,
 
Hakuna kilichoongezeka wala kukanushwa hapo zaid ameelewesha tu ili watu waelewe.
 
Hapo ni kukanusha au kufafanua mkuu?
Ni kanusho dhidi ya dhana iliyotaka kujemgwa kuwa sera mpya imeanzishwa wakati sera hii ipo siku nyingi. Kama ilikuwa haitekelezwi wala kufuatwa, sasa itatekelezwa kama inavyotakiwa.
 
Mbona wengi tu wako masomoni na mshahara unasoma? Ina maana hiyo standing order haikuwapo?
 
Kwahiyo mtu akienda kusoma first degree atapata mshahara au hapati
 
yaani hapo kaboresha maelezo na sio kakanusha..mana ktk ile barua yote yapo bora angekaa kimya...#team kufanya kazi kwa uwoga#
 
Ndo tatizo, maofisa wa serikali kukurupuka kutoa taarifa/waraka bila kujiridhisha ujumbe utaeleweka kwa walengwa au la.

Maana kila siku tunasikia ''ufafanuzi'' baada ya taarifa/waraka, hakuna kitu kinatolewa kama taarifa kwa umakini na usahihi huku ukijali kama wasomaji au walengwa wataelewa taarifa hiyo kwa usahihi.
huu hupotoshwaji unafanywa na wahuni, bila kujua wakidhani wanaichafua serikali, watasumbuka sana
 
Back
Top Bottom