Yaani umeandika mambo mengi kwa kufoka! Haya mtoto bado ni mdogo anahitaji malezi ya karibu hasa ya mama, mwenzio hajasema kama anaweza kulea mtoto wa umri huo, labda ana mke ni umalaya wake ulimpeleka huko nje mtoto akapatikana analea mtoto kama biashara ya bangi vile (kwa kificho) atambeba...
Basi mnafikiriaga ukiacha kumhudumia mtoto unamkomoa mama yake, kumbe unajaribu kujitenga na mtoto wako mwenyewe, haya huo ujeuri wa mama yake unakujaje bila wewe kusababisha? Mnaonaga vibanzi vya machoni pa wenzenu mnasahau maboriti yenu. Kuna story ndefu imejificha hapo upande wa pili
Wanafurahia pale wanapotafuta mali na wake zao afu majina wanaandika ya mama zao, dada zao, inapotokea wameshindwana mwanamke anabaki kutaabika, wabinafsi sana saivi wanamuona Haika jau kwenye jamii....wapo hawa marioo wa kulelewaga anamsogeza mwanamke karibuuu, taratiiiibu anaanza kumlaghai...
Ila nikawaza wauguzi wanavokuwaga saa zingine kuwa attend wagonjwa huwa wana madharau na kutokuchukulia jambo kwa uzito kama Dr alivyoagiza mpaka unatamani umpige, acheni apigwe labda apate adabu. Muuguzi alisababishaga kifo cha ndugu yangu wakahoji hoji pale sema mi naye nlikuwa nimeshachoka...
Maisha ni watu endana nao mkuu usifikiri wanaokula misibani ni njaa zinawafanya kula utawaza unavyowaza kwa nafasi uliyonayo katika jamii (labda bado ni mdogo hauna familia) na unafikiri misiba inawakuta kina fulani tu! Zamu itafika kwako ndiyo utajionea
Labda kwenye jamii yenu ndo wana njaa za hivyo, watu wanasusiwaga kila kitu mpaka faini itolewe, nimezunguka katika jamii nyingi Tanzania likimkuta mtu wa hivyo kwenye nzengo lazima kimrambe haijalishi kawapikia nini, kwanza anaanza kususiwa hakuna wa kupika, haya jamii nyingi mfiwa haruhusiwi...
Kukataa na kuvunja hizo imani kwa kuthubutu na kujiambia inawezekana kwa juhudi zote na bila kukata tamaa....ila ukianza mapambano ukakata tamaa na kurudi kule kule ayaaa ndiyo itakuwa gudubayi kwenye ramani ya maisha
Hata kama hana....ogopa walimwengu mkuu! Utafanya vile hata hawakuulizi wanasikilizia zamu yako ifike maana hii misiba ni kupokezana tu leo kwangu kesho kwako! Siku hiyo ndo utaorodheshewa yoote na hata kama hauna faini ndiyo utatoa ili watu washiriki kawaida msibani na wakule chakula chako, la...
Labda bado ni mtoto kwenye jamii/mtaa unaoishi hawakuchukulii kama mwananzengo mwenye mchango wowote kwao, hayo yafanye ukiwa mdogo kwenye jamii ila omba isifike zamu yako watu wakusanyike kwako! Siku hiyo ndo watataja tabia zako zoote na kukususia msiba wako. Imagine umefiwa na utatakiwa utoe...
Napenda maisha simple namna hiyo, harusi ni jambo la heri, linatakiwa kushehekewa bila kero, sio mtu anaoa/kuolewa anataka mambo makuuubwa ya kumshinda anaanza kuhangaisha watu na mimeseji ya mchango kila siku utafikiri anakudai, umekaa tu zako unapangilia mambo yako ghafla unajikuta kwenye...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.