Mkuu, utaitoa wapi amani kama unatoa uamuzi halafu wasomi wenzako wote wanakushangaa?
Sasa, kwa miaka yote hukumu yao itasomwa na kuchambuliwa na hadi watoto wa mwaka wa kwanza wa sheria na watakuwa wanawashangaa.
Ukiwa na amani katika hali kama hiyo, labda uwe mtu mjinga mjinga tu!
Hao majaji watakao mhukumu kifungo cha miaka mitano mtu aliyetiwa hatiani kwa kosa la uhaini, wataingia kwenye orodha ya majaji watatu wa ajabu Dunia haijapata kushuhudia.
Hoja yangu ni kwamba, uongozi wa CHADEMA na wanachama wake wanapaswa kuwa makini sana na kauli za hao kina Mange.
Kama taasisi itakubali kupelekeshwa na mtu mmoja tena kwa habari ambazo hazijathibitika, taasisi nzima itatumbukia shimoni.
Lema amekanusha na ana ushahidi, sasa huyo Hilda sijui ameleta ushahidi gani kuthibitisha anachosema.
Vijana wa CHADEMA wanatakiwa kuepuka sana unyumbu, hawa wanaharakati ni watu wa kuwa nao makini sana. Sio kila wanachosema akina Mange ni sahihi. Watakizika chama chao kwa uzushi.
Uongozi wao wa juu unawahusudu wanaharakati ambao kwa kiasi kikubwa wanaendeshwa na mihemko.
Hao wanaharakati wanaowaamini leo, 2030 kama watakuwa hai, watakuwa wakimpigia kampeni mgombea wa CCM.
Wanachadema wanakubali kuendeshwa na watu ambao hata hawana kadi za chama chao.
Kama uongozi wa juu wa CHADEMA utakubali kuendeshwa na kupelekeshwa na wanaharakati, chama kitapoteza uelekeo zaidi ya vile kilivyopoteza wakati wa Mbowe.
Kwa jinsi nilivyomsikia Lema, ni kama vile uongozi wa juu wa CHADEMA haukubaliani na baadhi ya uzushi wa akina Mange, ila unaogopa kuupinga...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.