Mada tunayoizungumzia ni nyeti na haihitaji ushabiki wa kisiasa. Katika suala hili tusizunguke kama paka anavyouzunguka ugali wa moto. Ukweli ni kwamba, katika suala la Zanzibar, tumeikosea demokrasia na kuonyesha ubabe katika maamuzi. Hakuna kitu ambacho hakifahamiki nje ya nchi yetu...
Ninaomba nijitose kuzungumzia angalao kwa kifupi suala zima la Wamarekani kutunyima msaada. Mambo mawili yametuponza. Sheria ya kubana uhuru wa habari na uchaguzi uliorudiwa Zanzibar. Sheria ya kubana uhuru wa habari ni mbaya ambayo huko mbele hata wale waliounga mkono kupitishwa kwa sheria hii...
Japokuwa inadhaniwa kuwa siri hiyo haijulikani, mioyo yao inawasuta sana. Yaani ni kwamba, watu wamemkataa Shein. Watu wameikataa serikali ya CCM. Sasa nchi itatawalikaje? Mioyo ya watu haimo na kiongozi wao. Hayo yatakuwa ndio matatizo ya ndani ya Zanzibar. Lakini kuna matatizo mengi zaidi nje...
Hapa tunahitaji kuwa makini sana. Ukweli ni kwamba, as far as I know, Kenya are more smart in business than Tanzania and for sure they know how to manipulate. Sisi tulikuwa a bit hesitant and slow. Lakini mimi ninampongeza sana Raisi wetu. Alipokutana tu na Museveni hakupoteza nafasi. aliutumia...
Japokuwa sina upande wowote ninaoegemea, ukweli ni kwamba CCM na serikali yake wamefanya kosa baya sana. Haki imepokonywa waziwazi na kiubabe. Haki imepokonywa na bila haki pia amani haiwezi kuwepo.
Ujumbe huu wa Askofu Kakobe si wa kupuuza. Barua yake kwa Raisi Kikwete ni ya terehe 10 Machi 2014. Lakini yanayotokea sasa huko CCM yamepatana kabisa na unabii wa Kakobe. Hapa kuna ujumbe kutoka kwa Mungu hivyo tusiweke ushabiki wa vyama wala wa madhehebu ya kidini.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.