Tunawaomba msitumie maneno makali kiasi hicho. Tuwe wastaarabu kidogo. Ombi kwa wale mnaochuja taarifa hizi kuwa makini kwa watu wanaotumia lugha chafu. Huyo anayeitwa zezeta humu ni mzazi wa watu.
Kwa uelewa wangu mdogo, wachambuzi wetu kabla hawajaruhusu ujumbe wenye viashiria vya uchochezi ama kwa namna moja ama nyingine maneno ya kukaraisha na kutia hasira, habari ambazo sio za kweli huchujwa. Je! Vipi katika hili?
Imekuwa kila kukicha tunaelezwa uzoefu wa mwalimu mpya wa klabu ya Simba kwamba ametokea katika kufundisha timu kubwa na kwamba anafahamiana na walimu wengi na wakubwa katika mataifa ya nje. Swali langu ni je; sifa na umaarufu wa mwalimu huyo unamchango gani kwa klabu ya Simba?
"Vodacom" Ngoma ikivuma sana, mwishowe hupasuka.
Mbali na kuwepo mipango mingi ya baadhi ya watumiaji wa mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom hapa nchini kuandaa wanasheria kwa lengo la kutaka kuifikisha kampuni hiyo mahakamani kwa kile wanachesema ni wizi kwenye vifurushi vya mtandao...
Ndoa kati ya kampuni za mitandao ya simu na serikali inayohusu tozo kwenye miamala mbalimbali inayofanywa kwa njia ya simu, pamoja na ndoa kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) zimekuwa ni ndoa kichomi kwa wananchi kutokana na mlundikano wa kodi...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.