Hili la Kipunguni kutolipwa fidia ya ardhi zaidi ya miaka 20 linafikirisha sana. Wananchi wanalipwa kwa awamu na kimakundi kidogo kidogo sana.Kulikoni! Uchaguzi ungekuwa wa huru na haki CCM ingepata shida sana Kipunguni. Hili serikali limalizeni.
Ninaafiki jeshi letu lifanye paradigm shift kwa kulinda mipaka ambayo dhana pana ni pamoja na raslimali za nchi dhidi ya maadui wa ndani na nje ya nchi. Mipaka ni uchumi,watu,ardhi na teknolojia ndani, vilindwe kwa wivu mkubwa.
C CM iwe makini kwenye kero za wananchi, kuteka na mauaji, raslimali za nchi,haki na wajibikaji na uongozi thabiti wenye kufuata katiba na sheria za nchi a la Mkapa hapo wataendelea kutawala, for sure. Ni hayo tu yanayowaangusha.
Mapinduzi au machafuko ni kitu kibaya sana ila mafisadi na pengo aliye nacho na asiyekuwa nacho inadhoofisha umoja wetu. Hali itakuja kuwa mbaya. Tunahitaji uongozi wa kukemea.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.