Mungu azilaze roho za marehemu peponi.
Nadhani serikali ikae na wakazi wa huko lazima taarifa watakuwa nazo. Iongee nao bila kutumia majeshi au polisi wenye silaha na wawasikilize wanataka nini kwa upole kabisa.
Pia, kutumia viongozi wa dini ni muhimu sana kuongea nao.
Wachangiaji tutoe maoni...
HII HALI SIYO NZURI KABISA KWA USALAMA WETU HUKO BAADAE.
NAONA LA MAANA WATU WENYE SOURCE ZA KUWASAIDIA POLISI WAWEZE KUTATUA HILI SWALA TUTUMIE HUU MTANDAO KUJADILI CHANYA ILI WAWEZE KUKABILIANA NAO.
HII TAARIFA NI SAWA ILA WATU KATIKA KUCHANGIA HUMU WASHAURI KULIKO KULAUMU JESHI LA POLISI...
Namshukuru rais kwa maamuzi yake magumu. Ni kweli hapo ni kuokoa maisha ya watu Mungu akubariki baba. Ila ningependa sana angesikiliza Mkurugenzi huyo wa muhimbili aliyefukuzwa na wizara wanasemaje kuhusu ubovu wa hizo mashine? Kwa nini waadhibiwe kumbe tatizo lilikuwa hazina kutoa b3 ambazo...
Hili jimbo litakuwa dalili liliuzwa haiingii akilini hata kidogo mgombea mmoja kurusha kwenye mtandao wake wa kijamii eti tumeshindwa. Nilishangaa sana. Sawa ni ustaarabu lakini uwe na madiwani wote wa kwenu halafu ubunge mkose????
Tutawasubiri kura za maoni hampati hata mmoja. mlifanya...
Nimesoma majadiliano sana na nikagundua Mr Rweyemamu hakusema amestaafu kwa mujibu wa sheria ipi? Amestaafu umri umefika miaka 60 kama watumishi wengine? Nadhani kama amefikia miaka 60 basi hiyo ni kawaida kabisa kama watumishi wengine wa umma. Siyo jambo la kujadili na kuunganisha na mambo...
Nami naunganika na wengine kuwa tunahitaji waziri wa fedha mzuri sana. Wengi wamependekeza na kwa picha naona wanamtaka mtu asiye mwanasiasa sana au hawafanyi maamuzi kwa nguvu ya wanasiasa kama Ludovick utouh. Wapo wengine pia Dr Idrissa Rashid, Kitillya(TRA). Mama Saada Mkuya alijitahidi kwa...
Ujumbe wako una pointi ya msingi kuwa Rais amesema tukimaliza kura ni vema tukarudi majumbani. Kama mkuu wa nchi anawajibika kulinda amani ya nchi na aiyache salama kama alivyokabidhiwa salama. ni busara ya hali ya juu sana.
Tatizo ilivyowekwa au kusomwa kwenye hotuba ya Mkuu ni haikunyooka...
Mzee mjanja sana. Hataki kwenda The hague yeye binafsi. Kama mtabeba ikatokea fujo yeye kashajitoa. Ni mfano nzuri kwa watu wengine wenye kusimamia vyombo nyeti kujiepusha maelekezo yatakayowaletea shida baadae. Nimemkubali kwa kuona mbali. Watu wengi wanajisahau kwenye kufanya maamuzi sahihi...
Hongera JK kwa kumuondoa huyo km wizara ya afya.
Haiwezekani Hospitali zote kubwa na ndogo nchi nzima kulalamika madawa halafu yeye bado haoni MSDimeshindwa kutekeleza majukumu yake. Serikali inapeleka hela MSD leo hii anaibuka mtu mmoja eti Hospitali zinunue dawa MSD. Hivi ni kiini macho au...
Nashauri serikali izuie mkutano huu maana wajumbe wa katiba wataamua. Hii ni vurugu maana wengine watafuatia.Pia, hotuba ya mheshimiwa rais ilipitiliza ingawa alisema ni maoni yake na chama chake, sasa inafanya kila chama kije na maoni yake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.