Kukubali wanafunzi wa kike kurudi mashuleni baada ya kujifungua ni kuwahamasisha kufanya ngono waziwazi. Mbona zoezi la kugawa kondomu mashuleni lilipokuja watu walipiga kelele ndiyo maana tunaona wasichana wenye umri mdogo wana watoto.
Mimi binafsi siungi mkono wao kurudi shuleni. Nyie mnaotaka...
Wizi wa simu Tengeru umepungua maana sasa hivi wale wanaofanya kazi ya bodaboda pale stendi wameingizwa kiwa polisi jamii. Zamani Tengeru ilikuwa inaongoza kwa wizi wa simu hasa siku za soko Jmosi na Jtano. Wale wachache waliobaki waache kabisa wakajishughulishe na kazi halali za kuwapatia kipato.
Tigo LTE ni uongo mtupu. Utakuta line inasoma 3G na iko slow kuliko. Mpango mzima ni Halotel. Sijui walikuwa wapi siku zote mpaka tukaibiwa na makampuni mengine
Hata mimi ilitokea hivyo hivyo. Nilijiunga na kifurushi cha shiling 3500/= lakini baada ya kupiga simu dakika 2 tu simu ikakatika na nikapata ujumbe kuwa sina salio la kupiga simu. Vodacom ni wezi sana. TCRA inatakiwa kuwafungia wezi kama hawa wanaoibia wateja wake.
Vodacom ni wezi kwa kwenda mbele. Kwanini wasilete utaratibu wao wa kutoa taarifa ya jinsi ulivyotumia pesa yako kwa matumizi ya simu mara tu unapokuwa umemaliza kupiga au kutuma sms.
Hao ni wezi wa hatari. Cha msingi acha kutumia mtandao wao basi.
Jamani naombeni msaada wa kwenye dish. Ku-PAS 7/10 (68.5) na C-intelsat 64E hazionyeshi channel tena. Au wamehama frequency? Anayejua naomba huo msaada maana hapa nimekwama
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.