1000 Japanese yen = 9
.1 US $ . Hivi hii inamaanisha pesa ya Zambia iko juu kuliko ya Japan. Thamani ya pesa inapimwa kwa nguvu yake sokoni sio ukubwa wa namba kwenye kubadilisha
Wanajeshi ni moja ya makundi ambayo hawaruhusiwi kuwa wanchama wa vyama vya siasa. Kwa Amirijeshi wetu mkuu mbona sio mwanachama tu bali kiongozi namba moja wa CCM. Bob Wangwe, Shangazi na wengine hebu tafuteni tafsiri mahakani kutokana na hatari iliyopo kwa kuchangany hizi nyadhifa
Sheria ya ajira na mahusiano kazini hairuhusu mtumishi kufanya kazi mfululizo kwa zaidi ya masaa 12. Huyo mwanasiasa anayeamrisha Dr. awe tayari kutumika masaa 24 anatambua hili? Serikali iangalie namna ya kuwaajiri madaktari wa kutosha sio kuwaadhibu hawa wachache wanajitoa kufanya kazi zaidi...
Ukitaka kujua wapi mtoto wako atapata elimu bora angalia viongozi wetu wanaosimamia elimu wanapeleka wapi watoto wao. Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako
Kosa la CAG kwa mujibuwa wakosoaji wake ni kuonyesha udhaifu wa bunge baada ya kuhojiwa na chombo cha nje. Hivi walitaka asijibu maswali kwa kuwa tu bado hajahojiwa na chombo cha ndani. Lakini kwa wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kuwa hii sio mara ya kwanza kwa CAG kueleza udhaifu huu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.