Pamoja kupata msiba mzito ndani ya familia, bado tuna nguvu ya kuweka visasi na vinyongo kwa watu wenye mawazo tofauti na sisi, hakuna funzo kabisa hadi tufe wenyewe?
Marekani pia anafadhiri Serikali ya Tanzania, majuzi tu Waziri wa Afya Mchengerwa kupitia wizara ya afya walituthibitishia hilo na wengine wengi na sekta nyingi sana
Nawaza tu ile mwitikio wa watu kwenye Tume ya Jaji Chande ulivyokuwa positive, kisha summary ya repoti ama hotuba ikawa vile na ripoti tukaambiwa sio public, hiyo nguvu inatoka wapi this time ya kwenda kutoa ushahidi ambao huenda nao tutaambiwa ni taarifa ya yangu niliyeunda tume yangu mwenyewe...
Uko sahihi kabisa, ingawa kwa kiasi kikubwa watesi wake wamejikuta wana rise political status yake na kushusha za kwao huenda pasipo wao wenyewe kujua hilo
Wakati wa kuweka jiwe la msingi walimtaja zikalipuka shangwe za kutisha, unajua waliopo ofisini wanavyoteseka na shangwe, kama imekuwa hivyo leo basi itakuwa sio kwa bahati mbaya hata kidogo
Binafsi naamini Lissu ni muujiza unaoishi duniani, amebeba hatima fulani, kupitia yeye nchi hii itaenda kupata mabadiliko mazuri hasa katiba mpya, tume huru ya uchaguzi nk. Natumai Mwenyezi analo kusudi mahususi kwake, litatimia siku moja hata kama itachukua muda. Na watesi wake wao wenyewe ama...
Mwenyezi Mungu ni wa Haki, nategemea kuona haki inatawala na tunalinusuru Taifa letu kutoka kwenye tension ya vyesi kila iitwapo leo. Inaonesha kwa sasa hata fedha za maendeleo zimepungua ili kugharimia vyesi mahakamani ndani ya nchi, ambapo washitakiwa ni raia wetu wenyewe, ambao walipaswa kuwa...
Nadhani gharama za serikili kwenye kuendesha vyesi itakuwa imepanda sana awamu hii, maana kila kukicha ni mashitaka mapya kila kona ya nchi na hivyo gharama za ulinzi hasa kupitia jeshi la polisi zitakuwa zimeshuti sana awamu hii.
Tunaendelea kupata fundisho kubwa, kamwe huko mbeleni tusikubali kuongozwa na viongozi vilaza wasiojiamini. Huu moto tunaopitishwa, hadi miaka hii iishe, sijui. Natamani kuona watu wakiweka vitendea kazi chini na wanafunzi wakose masomo wiki moja hadi 2, watoke mtaani, watawala waone...
Mungu yupi huyo anayezungumziwa hapa, hebu acheni kufuru basi. Mwenyezi Mungu kamwe hawezi kuleta kiongozi kwa njia ya kumwaga damu za watu wake, na baado hata sasa damu zinaendelea kumwagika na vitisho vya kupita kiasi kwa raia wa nchi yake mwenyewe
Jambo lolote ukilifanya kwa uonevu mwisho wa siku linamuinua mtendwa na kukudidimiza mtendaji wake, hata kama utamuua kimwili.
CCM kupitia dola hasa Polisi na wenzao wanachoifanyia Chadema, wamejikuta wao wanazidi kutokomea gizani ila watendwa wanashamili kila iitwapo leo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.