Recent content by Lukonge

  1. Lukonge

    JamiiForums Tanzania KERO Nimenyimwa Mafao yangu NSSF

    Mifumo inasomana/kuwasiliana ili kutambua wanachama, lakini hawahamishi data za mtu kutoka mfumo mmoja kwenda mwingine.
  2. Lukonge

    JamiiForums Tanzania KERO Nimenyimwa Mafao yangu NSSF

    Ukiwa na haki ya kupata fao lako lolote kwa mjibu wa sheria, kwa kuzingatia uko mfuko upi (PSSSF au NSSF), mfuko unaokulipa kwanza unakupatia barua ya kuwa umekulipa fao lako husika. Baada ya hapo, unatumia barua hiyo kwenda kwenye mfuko wa pili kufungua madai yako ili mfuko wa pili pia ukulipe...
  3. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Je, kujenga nyumba ya makazi bila kibali ni kosa? Kwanini watu wengi hufanya hivyo bila kusumbuliwa?

    Kuna vitu ambavyo halmashauri zetu zinafanya na kuviweka, ukiangalia uhalisia na kipato cha wanachi ni vigumu kutekelezeka kwa ufanisi na ni maumivu makali. Na UKIZINGATIA kibali husika kinakuwa hai ndani ya mwaka mmoja tu. Ina maana uwe umekamilisha ujenzi, sina uhakika kama walishabadili hili...
  4. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Je, kujenga nyumba ya makazi bila kibali ni kosa? Kwanini watu wengi hufanya hivyo bila kusumbuliwa?

    Naweza kutolea maelezo ya suala hili binafsi kama ifuatavyo kwa uzoefu wangu: Kisheria ni lazima na ni muhimu kwa pande zote mbili kutoa na kupata kibali cha ujenzi wa nyumba kwa eneo husika bila kujali limepimwa au halijapimwa na mipango miji au serikali. Sababu kuu ni kama ifuatavyo: 1...
  5. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Ni vigezo gani unatumia kutathmini ubora wa kazi iliyofanyika?

    Ubora wa kazi hupimwa kwa kazi husika kupitia kwenye mlolongo ufuatao: 1: Kuweka lengo la kazi husika/matokeo. 2: Kutanabaisha ubora wa kazi husika itakapokuwa imekamilika, unataka iwe na vigezo vipi? 3: Kutanabaisha hatua mahsusi za utendaji kazi husika na wahusika (SOP). 4: Kutekeleza kazi...
  6. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Mrejesho3,mtoto umri miaka 10 anakojoa mkojo umechanganyikana na damu

    Mashine ni hiyo hiyo, ila CUFF ya kuweka mkononi inakuwa ziko aina tofauti:
  7. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Mrejesho3,mtoto umri miaka 10 anakojoa mkojo umechanganyikana na damu

    Ni muhimu kuwa na kipimo cha kuweka mkononi kwa umri husika.
  8. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Mrejesho3,mtoto umri miaka 10 anakojoa mkojo umechanganyikana na damu

    Pole kwa kuuguza, Pamoja na kumwona daktari bingwa wa figo, ni vyema pia kuendelea kufatilia: 1: Ndani ya wiki alipoanza kuumwa kama alipata shida yoyote ya mafua, kikohozi au koo kwa ujumla. 2: Uzito wa mtoto tangu ameanza kuumwa kama unaongezeka kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida. 3: Pata sehemu...
  9. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Makonda: Sandaland akiendela na msimamo wake tutatoa Jezi kila mtu auze zake

    Tatizo ni sisi kuishi kwa hisia bila kuwa na taarifa kamili. Hatujui mkataba kati ya hizi tasisi mbili ukoje? Na pia: 1: Je Sandaland alipopewa mkataba aliondoka na kwenda kutengeneza jezi bila kuhusisha TFF kwenye mlolongo wa upatikanaji wa jezi husika? 2: Nani alihusika na kuchagua miongoni...
  10. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Ommy Dimpoz afunga comments Instagram

    Mambo ya kwenye kuta nne si rahisi kuyazungumzia kinagaubaga, tunazungumzia hisia tu. Labda kama uwe ulishawahi kuwa mhusika na unaweza kutoa ushuhuda.
  11. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Neno Zazwa ni Sawa na Zuzu?. Kukiukwa kwa Katiba ya JMT Huku Tumenyamaza, Je Sisi Watanzania ni Mazwazwa na Mazuzu?.

    Paskali, habari! Kwa taarifa yako sisi tumevuka hata huo Uzwazwa au Uzuzu, tulishaambiwa kuwa kwa nchi zetu za wakati huo: kulikuwa na wananchi wenye afya njema, wagonjwa na sisi huku ni maiti kwa mujibu wa Rais wa nchi jirani yetu hapa. Ni vigumu sana kulikwepa hili kimantiki kwa maana kuwa...
  12. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Je, mhitimu wa Diploma ya Clinical Medicine kusoma Bachelor of Procurement and supply chain management (Mzumbe) ina tija kwenye soko la ajira?

    Moja ya matatizo tunayokuwanayo ni kuichukua elimu kama siraha ya kusaka ajira tu. Lengo la elimu ni kupata uelewa wa kuja kuyasimamia mazingira yanayokuzunguka kwa kuitumia elimu husika na kwa wakati huo kutatua mahitaji ya maisha. Kumbuka ninazungumzia elimu na si vyeti, hapa atapanua uanda wa...
  13. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Kama unataka kuwa kupitia TAJIRI kupitia kuajiriwa basi usisome kozi ya UDAKTARI

    Moja ya kitu cha kukiainisha ni kuwa neno UTAJIRI ni subjective/hakuna kipimo cha moja kwa moja cha kusema hapa imeufikia utajiri. Kwa maneno ya jumla: Utajiri ni wingi wa mali, rasilimali, fedha, au vyanzo vya mapato ambavyo mtu, jamii, au nchi vinamiliki na kuzidi mahitaji ya kawaida ya...
  14. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Mkataba umeisha tarehe 31 Agosti. Leo tarehe 8 Septemba napigiwa simu na mwajiri kua haongezi tena. Wanasheria tafadhali

    Kisheria: Siku ya mwisho ya mkataba inapofika, pande zote mbili yaani mwajiri na mfanyakazi zinakuwa huru. Mfanyakazi halazimiki kwenda kazini. Tuzingatie HALAZIMIKI, maana kuna hiari hapo kama hakuna maelezo tofauti ya kikazi.
  15. Lukonge

    JamiiForums Tanzania Mkataba umeisha tarehe 31 Agosti. Leo tarehe 8 Septemba napigiwa simu na mwajiri kua haongezi tena. Wanasheria tafadhali

    Mtoa mada zingatia hapa, chochote kiendacho kinyume na sheria ya ajira na mahusiano mahala pa kazi ni batili. 1: Je mkataba wako haukuwa na kipengele cha kuongezwa kwa kuzingatia vigezo vya mwajiri? 2: Kitendo cha wewe kufika kazini na kutimiza majukumu kwa wiki nzima ndani ya ofisi baada ya...
Back
Top Bottom