Daaah, hii barabara changamoto kweli kweli. Tangu November 2024 mkandarasi bado anatafutwa. Na bajeti hii ya 2025/2026 bado anatafutwa. Tunaomba kujua sasa ni lini specific hii barabara itaanza kujengwa?? Nionavyo mimi mpaka huu mwaka unaweza kuisha tena. Mungu asaidie kwa kweli.
Hakuna mwenye majibu. Kila mmoja kaamua kukaa kimya. Hii barabara ilitangazwa June 2024, then ikatangazwa tena November 2024. Sasa ni miezi takribani 5 imepita bado ni kimya. Labda bajeti ijayo.
Nimesikitika kuona tenda iliyotangazwa mwezi June 2024 ikiwa na refence TR36/002/2023/2024/W/98 imetangazwa tena mwezi Novamba kwa reference namba TR36/002/2024/2025/W/88.
Shida iko wapi?? Kwani humu hakuna TANROADS wakatolea ufafanuzi?? Au ni danadana tu hii barabara ya Mbezi Victoria-Bunju...
Barabara ya Mbezi Victoria kwenda Bunju via Mpigi Magoe nayo ikumbukwe sasa.
Tunajua hii ni barabara ya TANROADS na tenda ilitangazwa mwezi June 2024 lakini mpaka sasa kimya. Taratibu za tenda zote hufanyikia kwenye mfumo wa NEST na kila hatua ni rahisi kuijua kwa kuona tenda imefikia wapi...
Tenda: TR36/002/2023/2024/W/98 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mbezi Victoria kuelekea Bunju kupitia Mpigi Magoe
Wakuu naomba kuelewa mchakato wa barabara ya kutokea Mbezi Mwisho kwenda Bunju kupitia Mpigi Magoe umefikia wapi?
Kinachonisikitisha hii tenda hata kwenye NEST ishatolewa na...
Wakati Mheshimiwa Mbunge wa Kibamba akichangia bajeti ya wizara ya ujenzi 2024/2025 alisema tangazo la tenda ya kujenga barabara ya Mbezi Victoria kwenda Mpigi Magoe limeshatoka.
Nimetafuta kila mahala hili tangazo sijaliona kabisa, ninachokutana nacho ni tangazo la barabara ya kibamba shule to...
Nimeshangaa sana hii barabara kukosa tena kwenye bajeti ya mwaka ujao. Sasa lami itakuwa ikiyatoa mabasi stand yakapita mbezi high school kidogo lami inaishia hapo.
Kwa kweli ni maajabu sana. Hivi kwa ubusy wa ile barabara kweli unaweza kuiacha kwa miaka kumi yote??!
Kwa kweli nimeshangaa na...
Wapendwa habari ya mapumziko. TANROADS nawasalimia sana kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naiomba wizara ya mali asili na utalii iziweke barabara za TANROADS mkoa wa Dar es Salaam katika list ya vivutio vya utalii, make na zenyewe ziko kiasili kabisa.
Barabara ni ya TANROADS tangu...
Nilichogundua hii barabara ni biashara ya watu. Haiwezekani ukwangue barabara tu alafu ulipe na baada ya siku tatu mashimo tayari. Tuwskwe wazi basi kwani wanaokwangua hawatakiwi kuweka vifusi?
Hizi taa mwanzoni zilikuwa zinaruhusu sekunde angalau kuanzia sitini. Kwa sasa wameamua kuweka sekunde ishirini.
Hii kwa kweli imerudisha foleni ya zamani. Sasa hivi foleni inaanzia njia ya kwenda UDSM. Huyu aliyeset hizi taa ana makusudi gani?
Hawa wanatapatapa tu, undeni Chato yenu iwe mkoa bila kuzigusa mikoa mingine. Tafuta clip ya JPM (RIP) akiwa Tunduru alafu mheshimiwa diwani na wewe utuletee hiyo aliyotoa ahadi hapo Chato iwe mkoa. Kwanza Chato ina hadhi gani ya kuwa mkoa?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.