Matundu ya choo na mafuta ya kula ni issue leo mnataka kupigana na Rwanda, kama mnataka kula ugali kwa mgawo na kutolipwa mishahara lianzisheni na Rwanda, nina uhakika ma man kagame atawafundisha na hamtarudia tena na vita za kichokozi kama Nyerere alivyomfundisha Iddi Amin
Naunga mkono hoja, weusi siku hizi wanamjua kristo kuliko wazungu waliowaletea, wazungu wengi waneshaacha hata kuamini hizo dini na kanisani wameacha kabisa kwenda, na kuna wale masheikh weusi wanamjua mtume kuliko waarabu na wako tayari kufa kutetea uislam
Uchawi ungekuwa wa kweli biashara ya Bank ingekufa, hakuna uchawi ni michezo tuu kama mazingaombwe, na wachawi 99% ni mafukara wa kutupa hata ugali maharage kwao ni issue
Pole ndugu, ni rahisi sana kuanza kuingia kwenye hayo mambo ya kiimani ukipata matatizo, be strong na jaribu sana kushughulikia kila tatizo separate bila kuunganisha na lingine, na mara nyingi kwa experience yangu ukipata tatizo moja basi mengine yanafuata mpaka unaanza kujiuliza nina mkosi...
Oa hata kumi, kwa Tanzania hakuna sheria inazuia kuoa zaidi ya mke mmoja, ila kama ni mtu wa imani itategemea uko upande gani maana wengine unaweza kuoa zaidi ya mmoja (waislam) na wengine hawaruhusu kuoa hata mmoja ( Ukiwa padri wa katoliki huruhusiwi kuoa kabisa)
Ibilisi ni kama ngano za alfu lela ulela tuu, hata babu yangu alikuwa nazo nyingi tuu na moja naikumbuka ilikuwa kuna kilima kimoja ukikipita lazima uiname mara tatu usipofanya hivyo unaweza leta mikosi kwenye ukoo
Aliyetufundisha kuhusu yesu na shetani ndio huyo huyo aliyefundisha jua linazunguka dunia na binadamu tuliamini hivyo for thousands of years mpaka scientist walipokuja prove sio kweli ni dunia ndio inazunguka jua, mambo ya imani ni magumu kidogo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.