Wapendwa,
Nilifanya online business name registration kwa BRELA toka 13/12/2016 lakini hadi leo bado hawajafanya clearance ya business name. Namba ya simu waliyotuwekea ukipiga haipokelewi na muda mwingine haipatikani kabisa. Naomba msaada wa mawazo wa namna gani naweza fanikisha huu usajili...
Kwa kijana yeyote wa kiume aliye songea mwenye kuhitaji kazi za kusimamia mashamba na shughuli za bustani anahitajika sifa ni
Awe tayari kuishi mashambani na wafanyakazi
Awe anafanyakazi kwa bidii
Mshahara atalipwa kila baada ya miezi mitatu lakini mahitaji yake ya muhimu yote juu ya mwajiri...
Kwa mfugaji wa kuku wa kienyeji aliyepo songea mjini nahitaji kununua tetea 80 na jogoo 8 kwa ajili ya kuwafuga, kama unao tafadhali wasiliana nami tufanye biashara hata kama unao chini ya hao tuwasiliane kwa pm.
Kama wewe unahitaji mzigo mkubwa wa mahindi kuanzia tani 100 kwa pamoja Fanya tuwasiliane mm nipo songea bei ya ubaoni kilo sh.500 mazungumzo yapo, karibu
Asanteni kwa michango yenu lakini kwa nini mnaleta lugha za kashifa bila kujua sababu zinazopelekea mtu kukosea katika uandishi? Ni typing error tu hapo, poleni hamjui mtendalo, na hata huyo anayesema niende kwanza shule kwani unanijua au,pole.
Wakuu salam, ninatafuta shule kwa ajili ya ndugu yangu form five kwa mchepuo wa CBG shule iwe mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma au Njombe iwe ni private yenye kufaulisha vizuri, iwe ni boys tu, kwa yeyote anayeijua anitajie na ada take, natanguliza shukrani kwenu nyote Asante.
Tatizo sio songea kuwa na mahindi mengi ila ni kuwa na bei itakayokuwezesha kurudisha gharama ya uzalishaji, ila usijali biashara ni mazungumzo ww unahitaji kwa bei
Gani?
Kwa wafanyabiashara mahindi yanapatikana songea yamekusanywa pamoja tayari kwa kuuza yapo zaidi ya gunia 1000 kwa mteja ambaye yupo tayari ajitokeze tuweze kupanga biashara ukusanyaji utakapo kamilika inategemewa kuwa na magunia yasiyopungua 5000 mnunuzi atakayekuwa tayari anakaribishwa sana...
Wakuu salamu, wataalam wa kilimo naomba mwenye document ya kilimo bora cha njegere maswala muhimu ikiwa ni namna ya kuandaa shamba, msimu mzuri wa kulima, nafasi kati ya mmea na mmea yaani formula ya upandaji, mbolea ya kutumia na mengineyo, asanteni.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.