Hiyo si sahihi Kwa suala la DRC. Ukipigana vita nchini DRC madini ya nchi hiyo yanaifadhili. Ndiyo maana nchi maskini kama Rwanda inaneemeka kupigana vita huko miaka nenda Rudi. Hata marekani wako tayari kufanya hivyo Kwa sababu wanajua kuwa kupigana vita huko inalipa. Hata sisi tungekuwa na...
Ni wavamizi Kwa sababu hata mazungumzo ya kuleta amani yanaihusu zaidi DRC na Rwanda na hao M23 ni misukule tu ya Wanyarwanda. Kama siyo jeshi la uvamizi hata mazungumzo yasingeihusu Rwanda.
Na siyo hiyo tu. Rwanda waking'olewa DRC nchi ya Rwanda itashindwa kujiendesha. Hata mishahara hawataweza kuwalipa watumishi wao. Kwa hiyo Rwanda hulichukulia suala la DRC kama ni la kufa na kupona.
Wako tayari hata kuua wacongo wote Ili serikali ya Rwanda isianguke Kwa kukosa pesa ya kuendesha...
Hii ya kulinda amani unaipata katika sheria ipi? Wanajeshi wetu hawakwenda kwenye mwavuli wa UN Bali Kwa mwavuli wa SADC Ili kupigana Kwa ajili ya mwenzake. Ukweli ni kuwa tulipigwa na M23. Mambo ya aibu sana
Siyo kweli kaka. Jeshi la SADC lilienda kupigana kumlinda member state mwenzake kama ilivyo kwa NATO wanavyofanya Kwa member state mwenzao. Hatukwenda kulinda amani Bali kuwatoa M23 na ndiyo sababu mkwara wa kwanza ilikuwa ni kupiga kunguru (M23). Inasikitisha kuwa tulipigwa kama watoto wadogo...
Mimi ninashindwa kuelewa. Nasikia kuwa Emily ni msomi na ni kijana kuliko nurdin. Iweje rais afanya hivyo wakati alituthibitishia kuwa uteuzi wake ni vijana wasomi? Hahahahaah
Hiyo Habari imepotoshwa na watutsi. Mheshimiwa mahiga hakuyasema hayo hapo juu. Angalia hapa alichosema
Listen to Minister Mahiga #np on #SoundCloud
https://soundcloud.com/willy-nyamitwe/minister-mahiga-didnt-say-what
Tanzania haikuwa inamkingia kifua Nkurunziza na pia haina uadui naye kama mlivyo nyie. HIyo ni tafsiri yako ya kimungiki mungiki. Maamuzi hubadilika kutokana na wakati pia na hiyo haitafsiriwi kama ni kuwa kigeugeu kaka!
Nadhani kazi mojawapo ya jeshi hilo la Africa iwapo litatumwa ni pamoja na kumsaidia nkurunziza kupambana na wakorofi kama Kagame na waasi anaowafadhili kupigana vita nchini Burundi. Nadhani kilichowavutia zaidi RSA na TZ ni pamoja na kuwa wale waasi wa m23 wanashirikiana na watutsi wa Burundi...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.