PAMOJA TUNALIA
Nalia nawe pamoja,mama tukimlilia,
Ni msiba sio hoja,jamvini metufikia,
Msiba si wa mmoja,wote tunamlilia,
Pamoja twamlilia,mama yako wetu sote.
La msingi zingatia,wosia lokuachia,
Malezi alokulea,mema yote shikilia,
Japo bado unalia,hekimaze zingatia,
Pamoja twamlilia,mama yako...