Kwa hiyo hata spika akipitisha uamuzi wa hovyo utakuwa kanuni? Kanuni si huwa zinaandaliwa na kujadiliwa kisha kupitishwa? Kama utaratibu ndio huu basi hakuna haja ya kuwepo kwa kanuni zilizoandikwa bali spika ndiyo awe kanuni.
ITABIDI niseme kile ambacho yumkini wengine wanakifikiria tu wakihofia kukisema: Mke wa Rais Kikwete, Salma Kikwete, si Rais wa Tanzania na wala si msaidizi wa Rais.
Yeye ni mwenza wa Rais na uhusiano wake na Rais unaishia kwenye masuala ya familia yake na mapenzi baina yao. Nje ya...
Nchi ya tume na kamati. Tume asubuhi, tume mchana, tume usiku, tume, tume, tume.......Iundwe tume ya kuchunguza ugonjwa unaowakumba Nape, Juliana na Mwampamba, wanasiasa waliofilisika wanaohubiri udini, ukabila, ukanda na ujinsia.
Mimi napendekeza Mark Mwandosya ambaye ni waziri asiye na wizara maalumu apewe WIZARA YA TUME NA KAMATI MAALUMU ili kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya tume na kamati maalumu lukuki zilizokwsha undwa. Mpaka sasa Tanzania naona ndio nchi inayoongoza duniani kwa kuund tume na kamati nyingi...
Safi sana Mbatia. Ungekubali tungekushangaa sana wakati hoja yako ya msingi waiikataa. Mimi nasema wewe ni tofauti sana na Zitto. Huyu Zitto aliongoza hoja ya mikataba ya madini bungeni mpaka aksimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge lakini la ajbu rais alipounda tume ya kuchunguza mikataba hiyo...
Ni jambo zuri hata kwa Tanzania. Siku ya uchaguzi isiwe Ijumaa, Jumamosi au Jumapili. Siku ya uchaguzi iwe ni Jumanne au Jumatano. Jumatatu mimi nafikiri pia sio nzuri kwasababu watu wanaweza wasipige kura kwa kuamua kusafiri(hasa walioajiriwa) Ijumaa au Jumamosi na kuwa safarini kurudi siku ya...
Mimi sioni kosa la Ndalichako na siamini kama anaweza kutoa maelekezo kwa wasahihishaji kusahihisha kinyume na maadili kwasababu za kisiasa. Tatizo la matokeo mabaya si la NECTA ni la mfumo wa elimu. Makosa ya kuchanganya majina hayawezi kuwa ndio sababu za matokeo mabaya. Uzuri baraza...
Mwanahalisi liliwahi kuandika habari ya kiuchunguzi inayoonesha uhusiano na mawasiliano ya siri kati ya Zitto na Mkurugenzi wa usalama wa taifa ambao kwa afya ya CHADEMA ulikuwa si mzuri. Katika hali hiyo si dhani kama Zitto atapenda gazeti hilo lifunguliwe kwa sababu lilishaanika baadhi ya siri...
Hivyo viti maalumu ni mzigo wa kujitakia. Wabunge wa viti hivyo hawana kazi wala umuhimu wowote na ni moja ya ishara ya ubaguzi ndani ya nchi. Kama sio ubaguzi kwanini kusiwepo viti maalumu kwa ajili ya wanaume, wazee na watoto?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.