Mbwa wazaa wengi, wazidiwaje na ng'ombe?
Swali hili ni la msingi, nijibu nipe ujumbe.
Najua hunipingi, wengi ng'ombe wenye pembe,
Wazidiwaje na ng'ombe, mbwa uzaaye wengi?
Mbwa ukizaa sita, ng'ombe mtoto mmoja,
Vipi ng'ombe wakupita mbwa kwenye mchakato?
Mbwa ni wengi mzalipo ni vipi mzidiwe...