habari zenu wapendwa wa jukwaa la lugha:
naendelea na kazi ya ufasiri kiswahili kwenda kiingereza... leo imebidi nifasiri "kiti cha marimba." je, "wooden chair" inatosha? au kiti cha marimba kina upekee fulani ambao haufikishwi kiingereza kwa kusema "wooden chair" tu? kama kawaida nitashukuru...
Wapendwa wanatovuti:
Mimi pia nitapenda kuwa nalo hilo kamusi...KLF inaonekana umefanya kazi kubwa. Kiungo kifuatacho huenda kikasaidia pia ni kazi iliyofanywa na wataalam wa UDSM (Institute of Computer Science na Institute of Kiswahili Research) na BAKITA...
Bi FaizaFoxy! Ama kweli wewe umenisaidiya sana tena sana na utaalam huo. Shukran zimiminike kwako. Kama hujachoka... utaweza kunisaidia neno lingine? - katika sehemu ya michezo ya watoto, kuna bembea, kunesa, na kuteleza. Nafahamu "swings" and "slides" lakini "kunesa" kwanishinda...
Waheshimiwa wa Jukwa la Lugha:
Natumaini hamjambo nyote. Mimi ni mfasiri wa Kiswahili kwenda Kiingereza. Leo nimekwama... ninahitaji kufasiri maneno hayo mawili: waya na seng'enge - katika maandishi nayoyafasiri kuna mtu anasubiri "waya na seng'enge" kuletwa.... waya si ni "wire"? seng'enge...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.