Waya na seng'enge, tofauti ilyopo tafadhalini

bi mgeni

Member
Apr 7, 2013
7
3
Waheshimiwa wa Jukwa la Lugha:
Natumaini hamjambo nyote. Mimi ni mfasiri wa Kiswahili kwenda Kiingereza. Leo nimekwama... ninahitaji kufasiri maneno hayo mawili: waya na seng'enge - katika maandishi nayoyafasiri kuna mtu anasubiri "waya na seng'enge" kuletwa.... waya si ni "wire"? seng'enge navyofahamu mimi ni "fencing wire" labda ya shaba, inayoviringishwa na kuwekwa juu ya kuta.... sasa nashindwa kuelewa tofauti iliyopo baina ya waya na seng'enge na sijui nifasiri vipi. "Wire and fencing wire" naona hai'sound'. Hiyo "waya" ina sifa gani? Mukiwezanisaidia nitashukuru sana.
Asanteni.
Bi Mgeni.
 
Ahsante Kinyungu. Samahani, naendelea kujikuna kichwa.
Kwa hivyo "waya" ndo vipi? "Smooth wire"? :rolleyes:
 
Sio lazima waya wa uzio (fence) uwe na miba (barbed).

Kwa hiyo waya wa uzio ni "fencing wire".
 
Seng'enge ni chainlink fencing au kwetu maarufu kama chicken wire au mesh wire. Zipo za aina tofauti.

Wire za kufungia hizo seng'enge zipo za aina tofauti. Zipo zile plain zinaitwa strainer wires na zipo zile za miba miba zinaitwa barbed wires.
 
Bi FaizaFoxy! Ama kweli wewe umenisaidiya sana tena sana na utaalam huo. Shukran zimiminike kwako. Kama hujachoka... utaweza kunisaidia neno lingine? - katika sehemu ya michezo ya watoto, kuna bembea, kunesa, na kuteleza. Nafahamu "swings" and "slides" lakini "kunesa" kwanishinda...
 
Bembea la kunesa nahisi unataka "seesaw swing".
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom