Kwa sasa kusini ni "hub" muhimu sana katika maendeleo ya nchi hii.
Huyo huyo Samia katoa bilioni 260 alizokopa toka AfDB kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya uchumi inayounganisha miji ya Mtwara, Nanyamba, Tandahimba, Newala hadi Masasi ambayo ina urefu wa kilometa 160.
Tunaposema "Kusini kuchele"...
Hawa polisi wa Tandahimba ni zaidi ya waporaji mkuu. Yaani wanazunguka hata majumbani na madukani kupora mapikipiki kisha huyapeleka kituoni ambako ukienda kufuatilia unapigwa faini kubwa ambayo itakuduwaza na hupewi hata EFD receipt.
Kiukweli askari wa Tandahimba ni wasumbufu sana kwa waendesha pikipiki. Nilienda likizo mwezi Agost mwaka huu. Siku moja wakati natoka kijijini naelekea Tandahimba mjini nikawakuta polisi wamesimamisha gari mikoroshoni halafu ghafla wakatokezea barabarani wakanizuia. Dah, ilikuwa mbinde yaani...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.