Hivi nani waliokuwaga nyuma ya mauaji ya ndugu zetu Albino awamu ya nne?

omtiti

JF-Expert Member
Jun 19, 2019
1,022
1,590
Nakumbuka kipindi cha serikali ya awamu ya nne yalikuwepo mauaji ya ndugu zetu Albino kwa wingi sana ,ikiwemo na vikongwe.

Hii ilipelekea aibu kubwa sana kwa taifa letu kwenye uso wa kimataifa, nakumbuka jambo hili lilimkera sana aliyekuwa waziri mkuu Mizengo Pinda mpaka ilipelekea kulia hadharani kwa uchungu.

Cha kushangaza baada ya awamu ya Tano kuingia Madarakani mauaji hayo yalikomeshwa kabisa,sijawahi sikia tena haya mauaji.

Tukubali tukatae mwendazake aliinyosha hii nchi kwa muda mfupi,hatukusikia cha majambazi kuvamia na kuteka,panya road walifutika,dawa za kulevya na mateja kupotea,na mengine mengi ambayo yalikuwa kichefu chefu awamu ya Nne.
Tutaendelea kumkumbuka mwendazake, maana waliotawanyika wanaanza kujongea ili wajikusanye kuendelea na uhalibifu wa raia na mali zao .wanaonekana kuwa na kiu sana
 
Mauaji ya albino yapo mkuu the thing is hayatangazwi na media tena kuepuka negative image ya nchi which is a good move.

Kuna nyuzi kule JF Habari mchanganyiko kuhusu experience za watu kuvamiwa na majambazi mbona watu wanafunguka tu walivyovamiwa tena wengine ni recent tu kipindi JPM yupo.

Changamoto ni media zetu hazichimbui habari zimekua za uoga uoga tu ndio ikafikia stage hadi watu wakawa wanapinga TZ haikuwahi kuwepo covid kwa hoja ya kwamba. Nitajie hata mmoja aliyekufa kwa covid???

China pia hujawahi sikia ugaidi sio kwamba haupo ila haupewi media coverage ili kuepusha negative image kimataifa.

Minya Media tu hakuna udhaifu utaonekana
 
Mwendazake nae ni wale wale tu tena yule alikuwa anauma na kupuliza halafu mwongo mwongo kinyamA jiwe
Raha ya Mwendazake alikuwa harembi ,rejea kuhusu issue ya mishahara ,alisema haongezi,Mama Samia kapita mlele kwa Lugha nyororo,je? Kaongeza ?
 
Mauaji ya albino yapo mkuu the thing is hayatangazwi na media tena kuepuka negative image ya nchi which is a good move.

Kuna nyuzi kule JF Habari mchanganyiko kuhusu experience za watu kuvamiwa na majambazi mbona watu wanafunguka tu walivyovamiwa tena wengine ni recent tu kipindi JPM yupo.

Changamoto ni media zetu hazichimbui habari zimekua za uoga uoga tu ndio ikafikia stage hadi watu wakawa wanapinga TZ haikuwahi kuwepo covid kwa hoja ya kwamba.... Nitajie hata mmoja aliyekufa kwa covid???

China pia hujawahi sikia ugaidi sio kwamba haupo ila haupewi media coverage ili kuepusha negative image kimataifa.

Minya Media tu hakuna udhaifu utaonekana
Wacha kudanganya takwimu kuhusu uhalifu kipindi cha Magufuli ulishuka kwa kiwango kikubwa sana .
Nani alikwambia media ziliogopa kuripoti matukio ya ujambazi?
 
Upo sahihi kabisa kipindi cha mwendazake kulikuwa na matukio ya kutisha kuliko kipindi chochote lakini kinachofanya watu waone akukuwa na hiyo shida ni mwendazake alivyoamua kuminya uhuru wa habari kwa manufaa yake binafsi
 
Wacha kudanganya takwimu kuhusu uhalifu kipindi cha Magufuli ulishuka kwa kiwango kikubwa sana .
Nani alikwambia media ziliogopa kuripoti matukio ya ujambazi?
Ukiendekeza ushabiki huwezi nielewa..... Media ndio tool ya watu kufahamu uhalifu kama media zikilala wewe utajuaje? Unless uwe ndani ya polisi ndio utapata taarifa.

Mfano Kibiti nani alikua na taarifa za uhakika za kilichoendelea zaidi ya rumors tu na Azory gwanda alivyofanya investigative journalism akamalizwa afu unasema hamna anayetishwa?

Mtwara last year mwishoni yaliyotokea bila social media ungeyajuaje? Polisi wamekuja kukiri only baada ya video kusambaa otherwise ww usingejua lolote!!

Hivi kuna media bongo ilidiriki kuhoji alipokua magufuli days prior to his death? Mbona media zote duniani zilihoji kasoro za bongo? Bila media za kenya kuhoji kuna mtanzania angejua JPM amezidiwa na amekaribia kufariki?

Tatizo hamjui nguvu ya media kama watchdog ya taifa.... Mmekalia tu ushabiki
 
Nakumbuka kipindi cha serikali ya awamu ya nne yalikuwepo mauaji ya ndugu zetu Albino kwa wingi sana ,ikiwemo na vikongwe.

Hii ilipelekea aibu kubwa sana kwa taifa letu kwenye uso wa kimataifa, nakumbuka jambo hili lilimkera sana aliyekuwa waziri mkuu Mizengo Pinda mpaka ilipelekea kulia hadharani kwa uchungu.

Cha kushangaza baada ya awamu ya Tano kuingia Madarakani mauaji hayo yalikomeshwa kabisa,sijawahi sikia tena haya mauaji.

Tukubali tukatae mwendazake aliinyosha hii nchi kwa muda mfupi,hatukusikia cha majambazi kuvamia na kuteka,panya road walifutika,dawa za kulevya na mateja kupotea,na mengine mengi ambayo yalikuwa kichefu chefu awamu ya Nne.
Tutaendelea kumkumbuka mwendazake, maana waliotawanyika wanaanza kujongea ili wajikusanye kuendelea na uhalibifu wa raia na mali zao .wanaonekana kuwa na kiu sana
Una akili kubwa sana. Umeona vyema. Hebu gusia kidogo kwenye masuala ya ujangiri alivyogusa
 
Back
Top Bottom