Smart sawa, ila kubwa kuliko ni uungwaji mkono kutoka kanda ya ziwa.
Kanda ya ziwa ni ya moto, ni eneo kubwa, lenye watu wengi, wenye moyo mkali (Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Kagera, ukiongeza na sehemu kadhaa za Tabora).
Wanaichukia serikali yao na vyombo vyake kama polisi, na kiongozi akiwa wa dini ile ndio anatazamwa vibaya sana kama namba moja na RPC Jumanne aliyetoa taarifa potoshi ya uchunguzi wa awali....Kwa kweli zamani ilikuwa ni kama hakuna udini ila sasa umewakaa (mwana kulitafuta mwana kulipata).
Katika jambo ambalo nakutana nalo wazi wazi ni chuki kali sana kutoka kwa wakristo na hususani wakatoliki (mtaani, serikalini, wapinzani, wana CCM) kufuatia tukio la kushambuliwa kwa Padri Kitima, tena kwenye makazi yake 'TEC HQ'.
Hao wasaka tonge wanao jiita G55 kwa kuwa walishatoka CHADEMA, kwa njia ya kuvuliwa uanachama na kujivua wao wenyewe hawana haki ya kutumia alama za chama (nembo, rangi, nk.).
Pia wazisambaze kwenye balozi za western; mabunge ya nchi za western; western media kama BBC, Sky News na CNN; mashirika ya kimataifa ya misaada ya sekta ya afya, elimu na ya kibajeti.
Uchafu wa Dola na Chama Cha Kijani unaumiza watu wa makundi yote ujue hilo.
Kuna wakatoliki, waluteri (Mbowe kwa mfano alivyowekwa kokoroni), waislamu (Marehemu Ali Kibao), hata wasabato nao watakuwemo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.