BMK lilianza kwa kasoro za hapa na pale lakini kubwa zaidi ni kitendo cha kundi linaloitwa UKAWA kuamua kususia mchakato mzima.Je matokeo yatakayopatikana baada ya BMK kumaliza mchakato yatakuwa halali?Kwa nini baadhi ya watu wanakosa usingizi kwa ajili ya UKAWA?Nasikia watapita kila...
Be realistic.Watu waliomchagua Raisi kwenye uchaguzi uliopita ni 4.5m kati ya Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura,mbona hamkusema Raisi asipite kachaguliwa na watu wachache?Tafakari.
Kwa kweli tusubiri tuone hatima ya yote.Kwa upande wangu ningependa zoezi zima lisitishwe,kabla mpasuko haujawa mkubwa.Wahusika wanatambua kuwa zoezi limefeli ila wanashindwa kusitisha kutokana na gharama zilizotumika.
Kwa namna mambo yalivyo katika Bunge la Katiba ni wazi kwamba zoezi hili limekwisha ingia dosari.Uzinduzi wake ulionekana kuwa wa kichama zaidi badala ya kubeba sura ya kiserikali,na huo ndio ulikuwa mwanzo wa kuharibika kwa zoezi zima.Je kwa namna mambo yalivyo tunategemea Katiba ijayo kuungwa...
Hatimae Mh Samuel Sitta amechaguliwa Kuwa m/kiti wa Bunge la Katiba, je utendaji wake utaweza kufanana ule wakati alipokuwa Spika?Sababu hakuweza kutetea nafasi yake kwenye kinyang'anyiro cha awamu ya pili ambapo Mh Makinda alishinda.Nini kipya ambacho unadhani atakuwa nacho wakati alionekana...
Mimi nilidhani hao watu 47,820 wamewakilisha wananchi wa makundi mbalimbali sababu kupata maoni kutoka kwa watu 45m moja moja nadhan zoezi lingechukua karne moja kukamilika.Je kwa mtazamo huo ina maana katiba tunayosubiri haitokani na maoni ya wananchi?Kwa hali hiyo ni kwamba tunajindanganya...
Nashukuru kwa muongozo wako.Kwa uelewa wangu mdogo nilifikir hao watu 45,000 unaotaja wamewakilisha makundi mbalimbali miongoni mwa wananchi.Ktk hili pia ningeomba unitoe hofu yangu.
Kutokana mwanzo wenye mashaka wa upatikanaji wa katiba mpya huenda Rais Kikwete akakumbukwa kwa moja wapo kati ya kuwa mwanzilish wa kupata katiba hiyo au kuanzisha mtafaruku wa kitaifa.Hii ni kutokana na jinsì CCM walivyooyesha kuwa kinyume na maoni yaliyopatikana.Sasa ukitumika hoja ya nguvu...
Ifike mahala sasa mahakama ziache kushughulika na migogoro ya vyama vya siasa.Vyama vya siasa vina miongozo au katiba zao,sasa inapotokea kutokuelewana kati ya mwanachama na uongozi wa chama basi matatizo hayo ni bora wakayamaliza wenyewe katika vikao vyao kuliko mahakama kupokea kero hizo, ili...
Ikiwa Chama tawala hakikubaliani na muundo wa serikali tatu na kuilaumu waziwazi tume chini ya mwenyekiti wake sidhani huko tuendeko kama tuatapata katiba mpya kwa amani.Hivyo nawasihi wadau wote kumaliza kwanza huu mvutano ambao tayari umejitokeza.Ukumbukwe kwamba maoni yaliyopatikana sio ya...
Nashindwa kuelewa ni kwa nini mahakama zinapokea migogoro ya vyama na wanachama wake.Mfano imetokea kutokuelewana kati ya mwanachama na uongozi wa chama,na chama kikiwa na katiba yake lakini mwanachama anapeleka tatizo mahakamani ikiwa vyama vyenyewe vina vikao vyake na vina katiba au miongozo...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.