Nawaza na kuwazua,
Iwe ndani au nje.
Niingie na kutoka,
Majivu yasibakie.
Iwe hapa au kule,
Ama mbali na karibu.
Nishinde au nishindwe,
Yasibakie majivu.
Kwa ngonjera pia tenzi,
Majembe pia vijembe.
Lugha hii naienzi,
Muweza nipiganie.
Nalala naweweseka,
Nikifika wanarudi.
Najenga...